-
Salami: Tutatoa kipigo kwa adui mpaka akubali kwamba hana ubavu wa kukabiliana na sisi
Jan 02, 2020 04:43Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Iran itatoa pigo kwa maadui mpaka iwafanye wakubali kwamba, hawana ubavu wa kupambana na taifa hili.
-
Jibu la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa tuhuma na vitisho vya Marekani dhidi ya taifa la Iran
Jan 02, 2020 04:30Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana asubuhi alihutubia hadhara ya maelfu ya wauguzi kutoka kila pembe ya Iran; na pamoja na mambo mengine, akaashiria shambulio la Marekani dhidi ya harakati ya Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq na kueleza kwamba, wimbi la chuki dhidi ya Marekani katika eneo na hasa nchini Iraq ni jibu na radiamali ya kawaida ya wananchi kwa jinai za nchi hiyo.
-
Tuhuma za Ujerumani dhidi ya Iran; mgongano katika misimamo na madai ya Ulaya
Jan 01, 2020 21:41Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, bila ya kutilia maanani siasa haribifu na za kichokozi za Marekani na nchi za Magharibi katika eneo la Asia Magharibi, imeitaka Iran eti ibadili siasa zake katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Kiongozi Muadhamu: Watu wa eneo hili wanaichukia sana Marekani
Jan 01, 2020 08:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinzudi ya Kiislamu akibainisha kwamba, 'Mimi, serikali na taifa la Iran tunalaani vikali shambulizi la Marekani dhidi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq', amesisitiza kuwa, watu wa eneo hili wanaichukia sana Marekani.
-
Iran yaitaka Marekani iachane na sera zake haribifu katika eneo
Jan 01, 2020 04:37Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameionya Marekani juu ya matokeo mabaya ya hatua zake haribifu na zisizo na mantiki katika eneo la Asia Magharibi.
-
Rais Rouhani awatumia viongozi wenzake duniani salamu za mwaka mpya 2020 Miladia
Jan 01, 2020 00:11Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe wa pongezi marais na viongozi na mataifa ya Wakristo kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Miladia wa 2020.
-
Rouhani: Watu wa Iran ni watiifu kwa mapinduzi na kiongozi
Dec 31, 2019 09:04Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Watu wa Iran ni watiifu kwa Mapinduzi, Kiongozi na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
-
IRGC: Vikosi na wananchi wa Iraq wana haki ya kujibu shambulizi la Marekani
Dec 31, 2019 03:55Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) sambamba na kulaani uvamizi uliofanywa na wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Iraq na shambulio walilofanya dhidi ya ngome za vikosi vya kujitolea vya wananchi vya wa nchi hiyo vya Hashdu Shaabi, limesema vikosi vya usalama pamoja na wananchi wa Iraq wana haki ya kujibu chokochoko hizo za Washington.
-
Dei 9, taifa la Iran latakiwa kuimarisha msimamo wake wa kupambana na ubeberu
Dec 30, 2019 09:44Washiriki wa maadhimisho ya "Dei 9" kote nchini Iran wametoa mwito kwa wananchi kuwa macho na kuimarisha msimamo wao wa kupambana na uistikbari kwani ni kwa njia hiyo ndipo taifa hili la Kiislamu litaweza kushinda vita vya pande zote vya adui.
-
Iran: Shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya vikosi vya Wairaqi ni kielelezo cha wazi cha ugaidi
Dec 30, 2019 08:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, uvamizi uliofanywa na wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Iraq na shambulio walilofanya dhidi ya ngome za vikosi vya kujitolea vya wananchi vya wa nchi hiyo vya al-Hashdu-Sha'abi ni kielelezo cha wazi cha ugaidi; na akasisitiza kwamba: Marekani inapaswa ikomeshe kuwepo kwake kivamizi katika eneo hili.