-
Wapalestina wasiopungua 94 wameuawa shahidi Gaza katika saa 24; 180 waaga dunia kwa njaa
Aug 04, 2025 07:10Vyombo vya habari vimetangaza kuwa Wapalestina wengine wasiopungua 23 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Jeshi la Yemen limeshambulia kwa droni maeneo matatu ya Israel katika kulipiza kisasi
Aug 04, 2025 04:08Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza operesheni kwa mafanikio kwa kuyalenga maeneo matatu ya kimkakati ndani kabisa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel). Jeshi la Yemen limetekeleza oparesheni hiyo kwa kutumia ndege tatu zisizo na rubani ( droni).
-
Zaidi ya wahamiaji 50 wafariki dunia katika boti iliyozama pwani ya Yemen
Aug 03, 2025 23:27Zaidi ya wahamiaji 50 wamefariki dunia na wengine hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji wa Kiafrika kuzama katika Bahari ya Arabia kwenye pwani ya Yemen.
-
Waziri Mkuu wa Pakistani: Ni haki ya Iran kuwa na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani
Aug 03, 2025 23:03Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani uvamizi haramu wa Israel dhidi ya ardhi ya Iran, akithibitisha haki ya Iran ya kuwa na mpango wa amani wa nyuklia.
-
Kutambua rasmi nchi ya Palestina: Hatua ya Kibinadamu au Mbinu ya Kisiasa?
Aug 03, 2025 22:57Abdel Bari Atwan, mchambuzi mashuhuri katika ulimwengu wa Kiarabu anasema kuwa, mpango wa kulitambua taifa la Palestina ni hadaa nyingine ya watetezi na waungaji mkono wa utawala ghasibu wa Israel unaoukalia kwa mabavu Quds Tukufu.
-
Wazayuni wavunjia heshima tena Msikiti wa Al-Aqwsa; Ben-Gvir akiwa mmoja wao
Aug 03, 2025 11:03Mamia a walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa na kufanya vitendo vya kichochezi katika eneo hilo takatifu.
-
HAMAS yamsuta Witkoff, yasema haitaweka chini silaha mpaka iundwe nchi huru ya Palestina
Aug 03, 2025 02:12Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekanusha madai yaliyotolewa na mjumbe wa Marekani Mashariki ya Kati Steve Witkoff kwamba ilionyesha nia ya kuwa tayari kukabidhi silaha zake wakati wa mazungumzo ya kusitisha mapigano Ghaza kati yake na Israel, ikisisitiza kwamba ina haki ya "kitaifa na kisheria" kukabiliana na uvamizi wa utawala huo wa kizayuni katika ardhi ya Palestina.
-
Nyaraka za UK: Mubarak aliidhinisha mpango wa US na UK wa 'kumdhalilisha' Saddam Kuwait
Aug 03, 2025 02:10Nyaraka za siri za Uingereza zilizowekwa hadharani hivi karibuni zimefichua kwamba rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, aliunga mkono mpango wa Marekani na Uingereza wa kumshinda kijeshi na kumdhalilisha Saddam Hussein wakati wa Vita vya Ghuba ya Uajemi, huku akitabiri pia kwamba kushindwa huko kijeshi kungepelekea kuanguka kiongozi huyo wa Iraq.
-
Wapalestina 1373 wauawa shahidi wakisubiri msaada wa chakula Gaza
Aug 02, 2025 23:07Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa: Tokea tarehe 27 Mei mwaka huu hadi sasa Wapalestina 1373 wameuliwa shahidi katika Ukanda wa Gaza wakati walipokuwa wakisubiri kugawiwa msaada wa chakula. Waliuliwa shahidi kwa kufyatiliwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni.
-
Pep Guardiola: Ubinadamu umetoweka mbele ya maafa ya Gaza
Aug 02, 2025 22:56Kocha wa timu ya soka ya Manchester City Pep Guardiola kwa mara nyingine tena amekosoa vikali ukimya wa walimwengu kuhusiana na jinai za utawala wa kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusema: "Ubinadamu umetoweka."