-
Hamas yajibu kimantiki bwabwaja mpya za Trump
Mar 06, 2025 06:28Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema upayukaji na vitisho vya Trump vinavuruga makubaliano ya kusitisha mapigano kwani vinauchochea utawala wa Kizayuni wa Israel kutotekeleza wajibu wake.
-
Utawala wa Kizayuni wafanya njama za kudhibiti misaada inayoingia Ghaza
Mar 06, 2025 06:28Maafisa kutoka mashirika matano makubwa ya misaada duniani na Umoja wa Mataifa wameonya leo Alkhamisi asubuhi kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuchukua udhibiti wa moja kwa moja wa misaada ya kibinadamu inayoingia kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
HAMAS yakaribisha mpango wa Waarabu wa kuijenga upya Gaza
Mar 05, 2025 22:56Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha mpango wa kuikarabati na kuijenga upya Gaza, uliopitishwa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi za Kiarabu mjini Cairo, Misri. Mpango huo pia unakusudia kuzuia kuondolewa Wapalestinakatika eneo hilo lililo chini ya mzingiro.
-
Amnesty yataka kuchunguzwa jinai za kivita za Israel nchini Lebanon
Mar 05, 2025 22:56Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru juu ya mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya vituo vya matibabu, magari ya dharura na wafanyakazi wa afya nchini Lebanon, na kutaja hujuma hizo kama uhalifu wa kivita.
-
Kwa nini Iran inakaribisha upanuzi wa ushirikiano na Afghanistan?
Mar 05, 2025 22:56Majadiliano na mikutano ya maafisa wa Iran na Afghanistan yanaendelea kwa lengo la kupanua uhusiano na kutatua masuala kati ya nchi hizi mbili.
-
Yemen yaangusha ndege ya 15 ya kisasa ya kijasusi ya Marekani
Mar 05, 2025 06:30Jeshi la Yemen limetangaza kuangusha kwa mafanikio ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper baada ya kuingia katika anga ya nchi hiyo kinyume cha sheria na kufanya operesheni za kijeshi katika mkoa wa magharibi wa al-Hudaydah.
-
Mpango wa Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusu Palestina unapingana na matakwa ya Marekani na Utawala wa Kizayuni
Mar 05, 2025 04:43Viongozi wa nchi za Kiarabu, katika mkutano wao mjini Cairo, wamepinga mipango na njama za kishetani za Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kukataa hatua za kulazimisha uhamishaji wa Wapalestina.
-
Hamas: Kufunga vivuko vya Ukanda wa Gaza ni jinai ya kivita
Mar 05, 2025 02:40Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS imelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kufunga kwa siku tatu mfululizo vivuko vya Ukanda wa Gaza na kuitaja hatua hiyo kuwa inashadidisha kukiukwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ni jinai ya kivita.
-
Mkutano wa viongozi wa Arab League wapasisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza
Mar 05, 2025 02:38Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) umepasisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza na kutaka kutumwa wanajeshi wa kulinda amani katika eneo hilo.
-
Hamas: Tumejenga upya uwezo wetu kwa vita vyovyote vya siku zijazo
Mar 05, 2025 00:43Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS amesema kuwa, ingawa uamuzi wa kuanzisha tena vita kwa sasa unaonekana uko mbali, lakini harakati hiyo tayari imejenga upya uwezo wake wa kijeshi ili kukabiliana na vita vyovyote vile vya siku za usoni.