-
'Kuripua Israel hospitali pekee ya matibabu ya saratani Ghaza ni ugaidi wa wazi wa kiserikali'
Mar 22, 2025 07:47Kitendo cha jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel cha kuiripua na kuibomoa kikamilifu hospitali pekee ya matibabu ya maradhi ya saratani katika Ukanda wa Ghaza kimelaaniwa vikali kimataifa na kuelezewa kuwa ni kilelezo cha wazi cha 'ugaidi wa kimfumo wa kiserikali' wa utawala huo haramu.
-
'Uwanja wa ndege wa Ben Gurion hautakuwa salama mpaka uchokozi dhidi ya Ghaza utakapokoma'
Mar 22, 2025 07:41Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimetangaza kuwa Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa Israel sasa hauko salama kwa usafiri wa anga na utaendelea kuwa hivyo hadi uchokozi wa utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Ghaza utakapokomeshwa na vizuizi vya misaada lilivyoekewa eneo hilo la Palestina vitakapoondolewa.
-
Hamas yatoa wito kwa vyombo vya habari kupinga propaganda chafu za Israel
Mar 22, 2025 03:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito kwa Waarabu na Wapalestina kushiriki katika mapambano ya vyombo vya habari ili kukabiliana na propaganda na vita vya kisaikolojia vya Israel vyenye lengo la kuvunja irada na azma ya watu wa Palestina.
-
New York Times: Marekani haitaweza kuishinda Yemen
Mar 22, 2025 03:30New York Times limeandika kuwa Marekani haitaweza kutoa pigo kwa Yemen katika mashambulizi yake ya kichokozi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Abu Obeida: Yemen imeonyesha kuwa Gaza haiko peke yake
Mar 22, 2025 01:00Msemaji wa tawi la kijeshi la harakati ya Hamas amesema kuwa wananchi wa Yemen wamegharamika pakubwa kwa ajili ya kuihami Gaza, hata hivyo bado wanaendea kuwaunga mkono na kuwatetea watu wa eneo hilo.
-
Maelfu ya Wapalestina watekeleza Swala ya Ijumaa licha ya vizuizi vya Israel
Mar 21, 2025 09:04Takriban Wapalestina 80,000 wameswali Swala ya Ijumaa ya tatu ya mwezi wa Ramadhani hii leo katika Msikiti wa Al-Aqsa huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, licha ya vikwazo vya Israel na vituo vya ukaguzi kuwazuia maelfu ya waumini wengine kufika eneo hilo takatifu.
-
Yemen yaonya Marekani, Israel: 'Kinachokuja ni kikubwa zaidi'
Mar 21, 2025 04:31Harakati ya muqawama ya watu wa Yemen, Ansarullah, imeapa kwamba nchi hiyo itaongeza operesheni zake dhidi ya ngome za Marekani na Israel ili kujibu uchokozi wa Marekani dhidi ya ardhi ya Yemen na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina hasa mzingiro na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS yaisihi dunia: Msiiache Ghaza 'inayovuja damu' iyakabili 'mauaji ya halaiki' peke yake
Mar 20, 2025 23:56Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa ombi la kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha "uangamizaji kizazi wa kimpangilio unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwatesa kwa njaa makusudi Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza", jinai ambazo imesema, "zinafanywa kwa usaidizi wa kuaibisha wa kimaitaifa usioweza kuhalalishwa".
-
Tajiri maarufu wa US ashangaa mataifa ya Kiarabu kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari Ghaza
Mar 20, 2025 23:53Mohamed Hadid, mfanyabiashara tajiri, ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Palestina amehoji na kushangaa kwa nini mataifa ya Kiarabu na Kiislamu hayaingilii kati kukomesha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
-
Waziri wa zamani wa vita wa Israel: Tunakabiliwa na 'mgogoro mkubwa zaidi katika historia yetu'
Mar 20, 2025 23:52Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Moshe Ya'alon ametoa mwito kwa waandamanaji kuendeleza maandamano yao ili kuiangusha serikali ya Benjamin Netanyahu na kuhitimisha alichokiita 'mgogoro mkubwa zaidi katika historia ya Israel'.