-
Makundi ya muqawama yasisitiza kuunganisha juhudi ili kukabiliana na mashambulizi ya Israel
Mar 20, 2025 07:00Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) zimesisitiza juu ya haja ya kuunganisha juhudi makundi ya muqawama ya Palestina na nchi za Kiarabu ili kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuunga mkono mapambano ya ukombozi katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na kupinga mipango ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina.
-
Israel yaua watu wengine 71 katika mashambulizi dhidi ya Gaza na kuikalia tena Netzarim
Mar 20, 2025 06:56Ripoti zinaonyesha kuwa ndani ya saa 24 zilizopita wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 71 katika miji ya Beit Lahiya, Rafah na Khan Yunis, huku wengine wengi wakijeruhiwa.
-
Moto mpya wa vita wawashwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa msaada wa Marekani
Mar 20, 2025 06:22Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza yaliyoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari, utawala wa Kizayuni umeanzisha tena vita vya umwagaji damu dhidi ya eneo hilo lililoharibiwa na vita, kwa kufanya mashambulizi makubwa ya kinyama ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya mashahidi wa Kipalestina na kujeruhi wengine wengi katika ukanda huo.
-
San'a: Iran haiingilii hata chembe maamuzi ya Yemen
Mar 20, 2025 03:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesisitiza kuwa: Iran haingilii hata chembe maamuzi ya serikali ya San’a na kwamba operesheni za Yemen dhidi ya Wazayuni ni uamuzi huru na utaendelea kutekelezwa kivitendo hadi mzingiro wa Ghaza utakapovunjwa kikamilifu.
-
Saudia: Israel inahatarisha usalama na utulivu wa eneo zima
Mar 20, 2025 03:12Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatishia usalama na utulivu wa eneo hili zima na kwamba jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama zina wajibu wa kutekeleza majukumu yao ipaswavyo na kusimama kidete kukabiliana na hujuma za Israel huko Palestina na Syria.
-
Netanyahu: Mashambulio yalioua watoto 174 Gaza ni mwanzo tu
Mar 19, 2025 23:40Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kushadidi mashambulio mabaya dhidi ya Gaza, akionya kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya anga, ambayo yaliua watoto wasiopungua 174 katika ukanda huo, ni mwanzo tu wa uchokozi mkubwa zaidi dhidi ya Wapalestina.
-
Dunia yakasirishwa na hatua ya Israel kuendeleza vita dhidi ya Gaza
Mar 19, 2025 08:35Jamii ya kimataifa imebainisha hasira yake baada ya utawala katili wa Israel kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
-
Al Houthi: Israel inapanga kushambulia nchi zingine ikiwa itaangamiza Palestina
Mar 19, 2025 08:28Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuwa utawala ghasibu wa Israel utaanza kushambulia nchi nyingine ikiwa utafanikiwa kuangamiza juhudi za ukombozi za Palestina dhidi ya ukaliaji na uchokozi wake, huku akipendekeza hatua za kijeshi na nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya utawala huo.
-
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza
Mar 19, 2025 04:11Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.
-
Maafisa 5 waandamizi wa HAMAS wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel Ghaza
Mar 19, 2025 00:44Maafisa watano waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.