-
HAMAS, Jihadul-Islami, Wabunge wa US wapinga na kulaani matamshi ya Trump ya kuipora Ghaza
Feb 05, 2025 02:56Matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba nchi hiyo itawahamisha Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza na kulitwaa na kulimiliki eneo hilo la Palestina yamelaaniwa na kukosolewa vikali ndani na nje ya Marekani.
-
Saudia yapingana na Trump, yasema msimamo wake kuhusu Palestina ni thabiti na hauwezi kubadilika
Feb 05, 2025 02:21Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesisitiza kuwa msimamo wa nchi hiyo kuhusu suala la kuundwa nchi huru ya Palestina ni thabiti, wa kimsingi na hauwezi kubadilika.
-
Corbyn: Israel inabeba dhima ya kuuawa Wapalestina ' 61,709' Gaza
Feb 04, 2025 23:11Kiongozi wa zamani wa Chama cha Leba nchini Uingereza, Jeremy Corbyn ameubebesha dhima utawala haramu wa Israel na wale ambao wanaendelea kuupelekea silaha utawala huo wa Kizayuni, kwa mauaji ya kimbari huko Palestina.
-
Wapalestina 79 waliotolewa kwenye jela za Israel walazimika kwenda kuishi uhamishoni nje ya nchi yao
Feb 04, 2025 08:22Afisa wa vyombo vya habari katika ofisi ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS inayoshuughulikia masuala ya mateka Wapalestina amethibitisha kuwa mateka 79 wa Kipalestina walioachiliwa huru na utawala wa Kizayuni wa Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka Ghaza wamewasili Cairo baada ya kufukuzwa na utawala huo na kuhamishiwa nchini Misri.
-
HAMAS yapongeza operesheni ya Ukingo wa Magharibi iliyoangamiza na kujeruhi askari kadhaa wa Israel
Feb 04, 2025 07:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imepongeza operesheni ya kulipiza kisasi iliyotekelezwa dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambako utawala huo ghasibu umeshadidisha hujuma na mashambulizi yake.
-
Kwa kuhofia 'Nakba II', nchi 5 za Kiarabu zaiandikia barua US kupinga mpango wa Trump kuhusu Ghaza
Feb 04, 2025 07:07Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano za Kiarabu na Afisa Mkuu wa Palestina wametangaza kuwa wanapinga pendekezo tata la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza na kuwatafutia makazi mengine katika mataifa jirani.
-
Kuongezeka mashinikizo dhidi ya watetezi wa Palestina nchini Marekani katika muhula wa pili wa urais wa Trump
Feb 04, 2025 05:40Kwa kuanza muhula wa pili wa urais wa Donald Trump, pamoja na vitisho na hatua za serikali yake dhidi ya waungaji mkono wa Palestina, mashinikizo dhidi ya watu hao na harakati za ndani ya nchi hiyo pia zimeongezeka kwa kiasi kikubwa.
-
Hamas yaukosoa utawala wa Kizayuni kwa kukwamisha utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano
Feb 04, 2025 04:01Kiongozi wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anaendelea kukwamisha utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano na kubadilishana kwa uhuru wafungwa na mateka.
-
Maelezo mapya ya Israel kuhusu kushindwa "Kuba la Chuma" katika oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa
Feb 03, 2025 23:19Jeshi la Israel limetoa maelezo mapya kuhusu kushindwa kwa mfumo wake wa ulinzi wa anga unaojulikana kama "Iron Dome" katika operesheni ya wanamuqawama wa Palestina ya kimbunga ya Al-Aqsa.
-
Amri ya Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa lilitolewa wiki mbili kabla ya Oktoba 7
Feb 03, 2025 07:01Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vinasema kuwa, vina ushahidi unaoonesha kwamba, Muhammad Deif, Kamanda Mkuu wa Brigedi za Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la HAMAS alitoa amri ya kutekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa wiki mbili kabla ya tarehe 7 Oktoba 2023.