-
Kuenea vuguvugu la wanafunzi dhidi ya Israel kutoka Chuo Kikuu cha Columbia hadi Oxford
May 18, 2024 00:28Wanachama wa jopo la elimu na wafanyakazi zaidi ya 500 wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wameandika barua ya kuunga mkono kambi ya mshikamano na matakwa ya wanafunzi wanaoandamana katika chuo kikuu hicho kuunga mkono Palestina na kulaani jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Idara ya Habari ya Gaza: Israel imeua zaidi ya maprofesa na wanasayansi 100
May 17, 2024 11:49Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Gaza imetangaza kwamba jeshi la Israel limeua zaidi ya wanasayansi, wasomi, maprofesa wa vyuo vikuu na watafiti zaidi ya mia moja katika vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza kwa mwezi wa nane mfululizo.
-
Yemen yatungua droni ya ujasusi ya Marekani yenye thamani ya dola milioni 30
May 17, 2024 11:45Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limeitungua droni ya ujasusi ya Marekani kwa kutumia kombora la kawaida lililobuniwa na Wayemeni wenyewe.
-
Wazayuni washambulia misafara ya misaada ya kibinadamu huko Gaza
May 17, 2024 05:54Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakishambulia malori yanayobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza karibu na mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah
May 17, 2024 04:46Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeripoti kuwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 13 wametia saini barua ya kuuonya na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa ardhini katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada zaidi kuwafikia Wapalestina.
-
HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni
May 17, 2024 04:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
-
"Kuna haja ya kuitetea Gaza katika Hija ya mwaka huu"
May 17, 2024 03:40Rais wa Chuo cha Da'awa ya Kiislamu cha Lebanon amesema ibada ya Hija ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee wakati huu ambapo Wazayuni wanaendelea kumwaga damu za Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, "Kuna haja ya kuitetea Gaza katika Hija ya mwaka huu."
-
Viongozi wa Kiarabu waondoka Bahrain bila ya msimamo wowote wa kuiadhibu Israel kwa jinai za Ghaza
May 17, 2024 03:40Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama uliofanyika nchini Bahrain wa kuundwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina na kuitishwa mkutano wa kimataifa wa amani, lakini imeshindwa kuidhinisha hatua yoyote ya kuuadhibu kiuchumi na kisiasa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Zaidi ya watoto 15,000 wameuawa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza
May 16, 2024 08:52Zaidi ya watoto 15,000 wanaripotiwa kuuawa shahidi na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
AFC yataka FIFA iifutie uanachama Israel kutokana na jinai zake Gaza
May 16, 2024 08:51Shirikisho la Soka Asia (AFC) limetangaza kuunga mkono ombi la Palestina la kulitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) liifutie uanachama Israel katika taasisi hiyo kubwa zaidi ya kandanda duniani, kutokana na utawala huo wa Kizayuni kutenda jinai kubwa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.