-
AFC yataka FIFA iifutie uanachama Israel kutokana na jinai zake Gaza
May 16, 2024 08:51Shirikisho la Soka Asia (AFC) limetangaza kuunga mkono ombi la Palestina la kulitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) liifutie uanachama Israel katika taasisi hiyo kubwa zaidi ya kandanda duniani, kutokana na utawala huo wa Kizayuni kutenda jinai kubwa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Maandamano ya Wazayuni dhidi ya Baraza la Mawaziri la Netanyahu katika Siku ya Nakba
May 16, 2024 05:47Moja ya matukio muhimu yaliyojiri katika Siku ya Nakba mwaka huu ni maandamano yaliyofanywa na Wazayuni wanaopinga vita dhidi ya Gaza. Wazayuni hao waliandamana mbele ya jengo la Wizara ya Vita ya Israel huko Tel Aviv.
-
HAMAS: Tumeangamiza askari 12 wa Israel katika 'operesheni tata' Jabalia, Ghaza
May 16, 2024 03:55Izzuddin-al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa wapiganaji wake wamewaangamiza wanajeshi 12 wa Israel katika eneo lililozingirwa la kaskazini mwa Ghaza.
-
Haniyah Katika Siku ya Nakba: Bila shaka Israel itatimuliwa Palestina
May 16, 2024 01:08Ismail Haniyah, Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema bila shaka utawala wa Kizayuni wa Israel hatimaye utaondolewa katika maeneo yote ya Wapalestina.
-
Marekani kukanusha tena kutokea mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza, ni kukana ukweli ulio wazi
May 16, 2024 00:55Licha ya Wapalestina zaidi ya elfu 35,000 kuuawa shahidi na utawala wa kigaidi wa Israel huko Ukanda wa Gaza, lakini Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House nchini Marekani amedai bila kuona haya kwamba serikali ya Rais Joe Biden haiyachukulii mauaji hayo kuwa ni mauaji ya halaiki.
-
Maelfu ya Wapalestina waandamana katika kumbukumbu ya siku ya Nakba
May 15, 2024 10:07Maelfu ya wananchi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu wameandamana kwa mnasaba wa Siku ya Nakba ambayo inakumbusha uvamizi, mauaji ya kimbari, ukatili na jinai za Wazayuni katika ardhi za Wapalestina.
-
Msemaji wa UNRWA atahadharisha kuhusu hali ya mji wa Rafah
May 15, 2024 08:34Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameitaja hali ya mji wa Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza kuwa sawa na mji uliotelekezwa uliosalia magofu.
-
Wapalestina elfu 10 wangali chini ya vifusi
May 15, 2024 08:29Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa Wapalestina elfu 10 bado wapo chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa katika mashambulizi ya jeshi la Israel.
-
Marekani na Uingereza zashambulia tena uwanja wa ndege wa al Hudaidah huko Yemen
May 15, 2024 08:20Ndege za kivita za Marekani na Uingereza kwa mara nyingine tena zimeushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa al Hudaidah huko Yemen.
-
Balozi wa Russia UN: Mashambulizi ya Magharibi dhidi ya Yemen ni kinyume cha sheria
May 15, 2024 02:38Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashambulizi ya muungano wa nchi za Magharibi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Yemen yamekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa na hayana uhalali wowote.