-
Israel yashadidisha ukatili, Wapalestina 450,000 waikimbia Rafah
May 15, 2024 01:05Umoja wa Mataifa umesema eneo kubwa la mji wa Gaza sasa limekuwa “Mji uliotelekezwa.” Hayo yaliripotiwa na mashirika ya umoja huo yanayoshughulikia masuala ya misaada ya kibinadamu siku ya Jumanne na kuongeza kuwa Wapalestina wapatao 450,000 wamelazimika kuondoka eneo la Rafah kutokana na kushadidi mashambulizi ya Israel.
-
Makumi ya Wapalestina wauawa katika hujuma za Israel Gaza
May 14, 2024 07:35Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina, wakiwemo watoto wadogo na wanawake.
-
Amir wa Qatar na Waziri Mkuu wa Malaysia wajadili uhusiano wa pande mbili na hali ya Gaza
May 14, 2024 03:44Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amekutana na kufanya mazungumzo na Anwar Ibrahim Waziri Mkuu wa Malaysia katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha. Waziri Mkuu wa Malaysia yuko nchini Qatar kwa ziara ya siku tatu.
-
Yemen yaonya inaweza kulenga shabaha za adui 'ambazo hawezi hata kuzifikiria'
May 14, 2024 03:20Jeshi la Yemen limeonya kuwa huenda likazidisha mashambulizi yake ya kuiunga mkono Palestina iwapo utawala wa Israel utaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
-
Sababu za kushindwa mazungumzo ya kusitishwa vita vya Gaza
May 14, 2024 00:08Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, amefafanua jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel ulivyovuruga mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na kubadilishana mateka.
-
Nasrullah: Wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya Gaza
May 14, 2024 00:07Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya utawala huo haramu dhidi ya Gaza, jambo ambalo limeyalazimu makundi ya muqawama katika eneo la Magharibi mwa Asia, ikiwemo Hizbullah, kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel ili kuilazimisha kukomesha vita hivyo.
-
Familia za wanajeshi waliouawa zamshambulia Waziri wa Usalama wa Israel
May 13, 2024 23:38Familia za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliouawa vitani Ukanda wa Gaza zimemshambulia Itamar Ben- Gvir Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni.
-
Balozi wa Yemen nchini Iran: Mkutano wa Tehran utaleta maelewano kati ya Iran na Waarabu
May 13, 2024 23:20Balozi wa Yemen nchini Iran amesema kuwa Mkutano wa Mazungumzo ya Iran na Waarabu uliofanyika mjini Tehran chini ya anwani "Kwa ajili ya Ushirikiano na Maelewano" utaliimarisha taifa la Palestina na kuboresha maelewano kati ya Iran, Waarabu na nchi mbalimbali.
-
MSF watahadharisha kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya ya binadamu huko Rafah
May 13, 2024 23:06Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imesema kuwa hali ya mji wa Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza ni mbaya.
-
Mfumo wa huduma ya afya wa Gaza unakaribia kusambaratika kabisa
May 13, 2024 08:30Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, ambayo inaendelea kustahamili vita vya mauaji ya kimbari vinavyotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika eneo hilo imeonya kuhusu kusambaratika kabisa mfumo mzima wa afya katika eneo hilo.