-
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu aonya kuhusu kushadidi kwa vita vya Gaza
Mar 04, 2024 23:09Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu kushadidi vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.
-
Ansarullah ya Yemen: Baada ya tuliyoizamisha, tutaendelea kuzishambulia meli za Uingereza katika Bahari Nyekundu
Mar 04, 2024 05:37Yemen imeapa kuwa itaendelea kuzishambulia meli za Uingereza katika Bahari Nyekundu ili kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, ambao wamekuwa wakiandamwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa muda wa miezi mitano sasa.
-
Kimya cha taasisi za kimataifa kuhusu kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Mar 04, 2024 04:34Licha ya kuendelea mgogoro wa Ukanda wa Ghaza na kushadidi jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina, lakini Umoja wa Mataifa na taasisi zinazohusiana na umoja huo hadi sasa zimeshindwa kuchukua hatua mahimu katika kutetea haki za Wapalestina.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Iran ilikuwa pamoja nasi bega kwa bega katika vita dhidi ya Daesh (ISIS)
Mar 04, 2024 03:39Waziri Mkuu wa Iraq amesisitizia ulazima wa kutimuliwa wanajeshi wa kigeni wanaoongozwa na Marekani nchini humo na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni nchi jirani yenye mafungamano makubwa ya kidini na kijamii na wananchi wa Iraq, inaisaidia Baghdad katika vita dhidi ya magaidi wakiwemo wa Daesh au ISIS.
-
Kuongezeka mgawanyiko katika Baraza la Mawaziri la Vita la utawala wa Kizayuni kutokana na safari ya Gantz nchini Marekani
Mar 03, 2024 22:58Safari ya Benny Gantz, mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Vita la utawala wa Kizayuni huko Marekani imekosolewa vikali na Benyamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo.
-
Shehbaz Sharif ateuliwa kuwa waziri mkuu wa Pakistan baada ya uchaguzi wenye utata
Mar 03, 2024 08:53Shehbaz Sharif ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa Pakistan kwa mara ya pili, wiki tatu baada ya uchaguzi wenye utata uliopelekea kuundwa kwa serikali ya mseto.
-
Wanajihadi wa HAMAS wadhibiti ndege isiyo na rubani ya Israel
Mar 03, 2024 04:09Wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wametangaza habari ya kutwaa na kudhibiti ndege isiyo na rubani ya Israel (droni), ikiwa ni kuendelea kujibu jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Yemen: Operesheni katika bahari Nyekundu zinaendelea
Mar 03, 2024 01:07Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imesisitiza udharura wa kuendelezwa operesheni za vikosi vya majini vya nchi hiyo hadi hapo utawala wa Kizayuni wa Israel utakapositisha jinai zake huko Ukanda wa Gaza.
-
Israel yapuuza malalamiko ya dunia, yaendelea kumwaga damu za Wapalestina
Mar 02, 2024 08:19Kwa akali Wapalestina 17 wameuawa shahidi katika mashambulizi mapya ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyolenga nyumba tatu za Wapalestina katika maeneo ya Deir el-Balah na Jabalia katika Ukanda wa Gaza.
-
Amnesty International yataka uchunguzi wa mauaji ya waliokuwa wakisubiria misaada Gaza
Mar 02, 2024 04:01Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji makubwa ya Wapalestina yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Gaza waliokuwa wakisubiria kupokea misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.