Mar 05, 2024 02:39 UTC
  • Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu aonya kuhusu kushadidi kwa vita vya Gaza

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu kushadidi vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.

Volker Türk, amesema hayo alipokuwa akizungumza katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi na kusisitiza kuwa, ni muhimu kuepukwa kushadidi vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Aidha amesema, kuna ulazima wa kuepuka kushadidi vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwani kupanuka vita hivyo kunaweza kuwa na matokeo makubwa katika Asia Magharibi na kwingineko.

Licha ya kuendelea mgogoro wa Ukanda wa Ghaza na kushadidi jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina, lakini Umoja wa Mataifa na taasisi zinazohusiana na umoja huo hadi sasa zimeshindwa kuchukua hatua mahimu katika kutetea haki za Wapalestina.

Zaidi ya Wapalestina 30,000 wameuawa shahidi tangu Israel ilipoanzisha mashambulio yake ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana (2023)

 

Utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na serikali za Ulaya waitifaki wa Washington, umekataa kuwajibika kuhusu jinai zake na hivyo kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wasio na ulinzi huko Palestina.

Kufuatia operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba 2023, mashambulizi ya utawala wa Israel yameshtadi dhidi ya raia wa Palestina na miundombinu ya kiuchumi na afya, zikiwemo hospitali za eneo la Gaza.

Serikali za Magharibi ambazo kila mara zimekuwa zikidai kuwa ni watetezi wa haki za binadamu, zimekaa kimya kuhusiana na matukio ya hivi karibuni huko Ghaza na hali mbaya ya kibinadamu ya eneo hilo na kwa namna fulani kuhalalisha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

Tags