Jun 25, 2024 07:45 UTC
  • FAO: Iran kuzalisha zaidi ya tani milioni 20 za nafaka

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, uzalishaji wa nafaka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utazidi tani milioni 20 mwaka huu.

Shirika la FAO limesema katika ripoti yake mpya kwamba, uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini utaongezeka mwaka huu kutokana na sera ya kutegemea uzalishaji wa ndani badala ya kuagiza kutoka nje. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwaka jana ilizalisha tani milioni 19.8 za nafaka na hivyo kuwa nchi iliyozalisha kwa wingi nafaka barani Asia na wakati huo huo ilinunu kutoka nje tani milioni 14.9 za nafaka. 

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa pia limekadiria kuwa Iran mwaka huu itavuna tani milioni 13.5 za ngano sawa na mwaka jana.

Kuongezeka mavuno ya ngano Iran 

FAO pia imetabiri kuwa uzalishaji wa mchele hapa nchini utaongezeka kwa asilimia 18 na kufikia tani milioni 2.6 mwaka huu.    

Tags