Papa Leo: Kuundwa taifa la Palestina ndio suluhisho pekee la amani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133838-papa_leo_kuundwa_taifa_la_palestina_ndio_suluhisho_pekee_la_amani
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ambaye alikuwa safarini huko Beirut nchini Lebanon, amesema kwamba kuundwa taifa la Palestina ndio chaguo pekee linaloweza kuhakikisha haki kwa Wapalestina na Waisraeli.
(last modified 2025-12-02T09:06:31+00:00 )
Dec 02, 2025 06:55 UTC
  •  Papa Leo XIV
    Papa Leo XIV

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ambaye alikuwa safarini huko Beirut nchini Lebanon, amesema kwamba kuundwa taifa la Palestina ndio chaguo pekee linaloweza kuhakikisha haki kwa Wapalestina na Waisraeli.

Papa Leo amesema kwamba suluhisho la mataifa mawili ndilo chaguo pekee linaloweza kuleta haki kwa Waisraeli na Wapalestina.

Mwaka wa 2015 Vatican ilitambua rasmi taifa la Palestina na tangu wakati huo imekua ikiunga suluhisho la mataifa mawili.

Kauli ya sasa ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia ndio wito wake mkubwa zaidi wa kutaka Palestina itambuliwe rasmi na jamii ya kimataifa, wakati huu Israel ikiendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Papa Leo amesema: "Sote tunajua kwamba Israel haikubali suluhisho kama hilo kwa sasa, lakini tunaliona kuwa chaguo pekee. Vatican itabaki kuwa sauti ya upatanishi ili kusogea karibu na suluhisho lenye haki kwa wote."