Pezeshkian: Iran inasimamia nguvu ya Maadili na Uwajibikaji
-
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran inasimamia nguvu inayojali maadili na uwajibikaji huku akiwatuhumu maadui zake kwa kuwakilisha nguvu zisizo na uwajibikaji.
Akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa X, Bwana Masoud Pezeshkian amesema: "Iwapo siasa zitashushwa hadhi na kuwa nguvu tupu, basi matokeo yake ni ulimwengu tunaohuhudia sasa- uliojawa na machafuko, dhulma, ukosefu wa haki na uharamia.
Rais Pezeshkian ameongeza kuwa, katika utamaduni wa taifa la Iran na mfumo wetu wa maarifa ya kidini, nguvu bila maadili haina maana."
Amesema kwa mara nyingine kuwa, "Iran inasimamia nguvu ya maadili na uwajibikaji, na maadui zake wanawakilisha nguvu zisizo na uwajibikaji na zinazokosa majibu."