Papa Leo aendelea kuponda bwabwaja za Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138208-papa_leo_aendelea_kuponda_bwabwaja_za_trump
Mvutano kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Leo wa XIV kuhusu misimamo ya kupinga vita unaendelea kutokota.
(last modified 2026-05-06T11:06:30+00:00 )
May 06, 2026 10:52 UTC
  • Papa Leo wa Kumi na Nne
    Papa Leo wa Kumi na Nne

Mvutano kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Leo wa XIV kuhusu misimamo ya kupinga vita unaendelea kutokota.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Mehr likinukuu RT, Papa Leo wa Kumi na Nne siku ya Jumanne alijibu mashambulizi ya maneno ya Donald Trump dhidi yake, kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani , Marco Rubio huko Vatican.

Papa Leo amesema:"Dhamira ya Kanisa Katoliki ni kuhubiri Injili na kutoa mafundisho kwa ajili ya kufanikisha amani. Ikiwa mtu anataka kunikosoa kwa kuhubiri Injili, basi afanye hivyo kwa uaminifu. Ninatumai kwamba wayayasikiliza maneno yangu."

Misimamo ya Papa ya kupinga vita, hasa kuhusiana na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran imeibua hasira ya Trump. Hivi karibuni Kiongozi huyo wa Marekani alitumia madai ya mara kwa mara ya silaha za nyuklia kama kisingizio cha kuchukua misimamo dhidi ya Iran na Papa wa Kanisa Katoliki.  Awali pia Donald Trump alikuwa amesema hana haja ya Papa ambaye anapinga sera zake.

Waziri Mku wa Italia, Giorgia Meloni pia amekosoa kauli  za Trump dhidi ya Papa Leo akisema hazikubaliki.

Papa amekuwa akikosoa hatua za uhasama za Marekani dhidi ya Iran na kusema vitisho vya Washington havikubaliki.

Inatarajiwa kuwa Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atatembelea Vatican siku ya Alhamisi.

Papa wa Vatican hapo awali alikuwa amesisitiza kuwa: " Siwezi kuunga mkono vita." Vile vile Vatican imekemea vikali tabia na sera ya maafisa wa serikali ya Donald Trump ya kutaka kuhusisha vita vya nchi hiyo dhidi ya Iran na imani ya dini ya Kikristo.