Viongozi wa Iran na Iraq wasisitiza kuimarisha mahusiano ya kimkakati
-
Rais PRais Masoud Pezeshkian wa Iran na Waziri Mkuu wa Iraq, Ali Falah al-Zaidi
Viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq wamesisitiza juu ya mafungamano marefu ya kihistoria, kiutamaduni, kidini, na ya kijamii yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, wakibainisha ulazima wa kuhifadhi na kuimarisha rasilimali hii yenye thamani kuu kama nguzo imara ya kutanua ushirikiano wa kimkakati.
Hayo yamebainika katika mkutano baina ya Rais Masoud Pezeshkian wa Iran na Waziri Mkuu wa Iraq, Ali Falah al-Zaidi ambaye yuko Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu. Wawili hao wamejadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu ya maslahi ya pamoja kwa nchi hizo mbili na njia za kuendeleza na kukuza mahusiano ya pande mbili.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri Mkuu wa Iraq, wakirejelea makubaliano ya pamoja kati ya nchi hizo mbili, wameichukulia kasi ya utekelezaji kamili wa makubaliano hayo kuwa hatua muhimu katika njia ya kuinua mahusiano na kulinda maslahi ya pande zote. Wamesisitiza hitaji kufanikisha uwezo wa pamoja katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kibiashara, usafirishaji, nishati, na ushirikiano wa kikanda.
Pande zote mbili, kwa kusisitiza umuhimu wa muungano na uratibu wa kudumu, zimetathmini kufungua upeo mpya wa ushirikiano kama dharura ya kimkakati kwa mustakabali wa mahusiano kati ya Tehran na Baghdad.
Aidha Rais wa Iran na Waziri Mkuu wa Iran wamebaini kuwa kukuza mahusiano ya pande zote, mbali na kuimarisha utulivu, usalama, na ustawi wa nchi hizo mbili, kutachangia pia katika kulinda maslahi ya mataifa haya mawili ndugu na kuimarisha mshikamano na umoja wa kikanda.