-
Euro-Med: Israel imeifanya njia ‘salama’ kuwa mtego wa kuua wakimbizi wa Gaza
Feb 25, 2024 23:34Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini Geneva limesema utawala wa Israel umegeuza njia inayodaiwa kuwa salama, ambapo watu wa Ukanda wa Gaza wanaweza kusafiri kuelekea kusini mwa eneo hilo, kuwa mtego wa kuwaua Wapalestina waliokimbia makazi yao.
-
Iran: Mataifa ya Kiislamu yachukue hatua za kuwanga mkono watu wa Gaza
Feb 25, 2024 07:43Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema mataifa yote ya Kiislamu yana wajibu wa kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kuwapa usaidizi wa kivitendo ili kuwafanya waondokane na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili.
-
Ngome za Israel zanyeshewa kwa 'mvua' ya makombora ya Hizbullah
Feb 25, 2024 06:25Wanajihadi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebaon wameshambulia kwa makombora na maroketi kambi kadhaa za utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu usiku wa kuamkia leo.
-
Askari wasiopungua sita za Kizayuni waangamizwa na Wanamuqawama wa Palestina Khan Yunis
Feb 24, 2024 23:09Brigedi za Mujahidina wa Palestina zimetangaza kuwa zimewaangamiza wanajeshi kadhaa wa Kizayuni katika operesheni ya karibuni zaidi iliyotekelezwa na Muqawama wa Palestina magharibi mwa Khan Yunis.
-
Qatar yalaani mbele ya Majaji wa ICJ undumilakuwili unaofanywa katika sheria za kimataifa
Feb 24, 2024 23:09Qatar imeiambia Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwamba inapinga kile ilichokiita "undumilakuwili" na uwepo wa nyuso mbili, kwa sheria za kimataifa kutumika kwa baadhi, na kutotumika kwa baadhi ya wengine. Qatar imetoa kauli hiyo wakati wa kusikilizwa kesi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Kuvunjwa UNRWA; Mpango wa upotoshaji wa Netanyahu kwa ajili ya kuepa kushindwa
Feb 24, 2024 22:57Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amewasilisha kwa kile kilichotajwa kama Baraza la Mawaziri la Usalama la utawala huo mpango wa kulivunja Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) ili kuepa taathira za kushindwa mbele ya makundi ya muqawama ya Palestina katika kipindi baada ya vita.
-
Hamas: Ndege za Marekani zinashiriki mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina Gaza
Feb 24, 2024 07:15Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema Marekani inatumia ndege za ujasusi katika Ukanda wa Gaza ili kusaidia katika vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo hilo.
-
Mamilioni ya Wayemen waandamana katika mshikamano na Wapalestina wanaodhulumiwa Gaza
Feb 24, 2024 07:14Mamilioni ya Wayemeni wameandamana kote katika nchi yao kuonyesha uungaji mkono kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wanakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vya utawala dhalimu wa Israel.
-
Ehud Olmet: Lengo la Netanyahu ni kuwapora Waislamu Msikiti wa Al Aqsa
Feb 24, 2024 02:48Waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni amefichua kuwa, Ghaza ni hatua ya mwanzo tu ya baraza la vita la Benjamin Netanyahu kwani lengo lao kuu ni kuwafukuza Wapalestina wote, huko Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kuwapokonya Waislamu Msikiti wa al Aqsa na kuziingiza ardhi hizo ndani ya maeneo mengine yaliyopachikwa jina la Israel.
-
Idhini mpya ya Uingereza kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya umati dhidi ya wananchi wa Palestina
Feb 23, 2024 04:57Uingereza ambayo ni moja ya waungaji mkono wakuu wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina sambamba na Ujerumani na Marekani, hivi sasa imetoa idhini mpya kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina hasa wa Ghazza. Madola hayo matatu ya Magharibi ndiyo yaliyoko mstari wa mbele katika kuusheheneza silaha hatari utawala wa Kizayuni ili uzidi kuua raia wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.