-
Ansarullah: Vikosi vya Yemen vina 'hamu' ya kukabiliana na US Bahari Nyekundu
Dec 30, 2023 06:55Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Ansarullah ya Yemen amesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vipo tayari kuingia katika makabiliano ya kijeshi na Marekani iwapo hali ya taharuki itashtadi katika Bahari Nyekundu.
-
Kuendelea mashambulio ya muqawama wa Iraq dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani
Dec 30, 2023 04:05Kufuatia kuendelea mashambulio ya muqawama wa Kiislamu wa Iraq dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani, vyanzo vya habari Ijumaa usiku viliripoti kushambuliwa vituo vingine vya kijeshi vya Marekani mashariki mwa Syria na kaskazini mwa Iraq.
-
Mauaji ya watoto huko Gaza; Kazi ya siku zote ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 30, 2023 03:44Ripoti iliiyotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema kwamba mwaka 2023 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa watoto katika Ukingo wa Magharibi.
-
Idadi ya waliofariki Gaza katika mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7 imefika 21,500
Dec 29, 2023 23:15Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na jeshi katili la Israel huko Gaza tangu Oktoba 7 imeongezeka hadi 21,507, huku 55,915 wakijeruhiwa.
-
Taasisi za kimataifa zaelezea wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza
Dec 29, 2023 22:59Kuendelea vita vya kikatili na jinai zinazotekelezwa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza kumeamsha hasira na wasiwasi wa tasisis za kimataifa kuhusiana hali mbaya na ya kusikitisha ya kibinadamu katika ukanda huo.
-
Ansarullah ya Yemen: Maji ya Kimataifa ni salama kwa meli zote isipokuwa za utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 29, 2023 06:59Harakati ya Muqawama wa Kiiislamu ya Ansarullah ya Yemen imesisitiza kuwa njia za majini za kimataifa ni salama kwa meli zote, isipokuwa meli za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel au zile zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
-
UNICEF: Idadi ya watoto Wapalestina waliouliwa na Israel Ukingo wa Magharibi pia haijawahi kushuhudiwa
Dec 29, 2023 05:57Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini amesema, idadi ya watoto Wapalestina waliouliwa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mwaka huu huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Baitul Muqaddas Mashariki ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa kila mwaka katika eneo hilo.
-
VIDEO: Askari Mzayuni akiri kuwaua makusudi watoto wa Kipalestina Gaza na anasaka mtoto mchanga pia ili amuue
Dec 29, 2023 03:37Askari mmoja wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amekiri kwa fahari kuwa anamsaka mtoto mchanga wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza ili amuue.
-
Uhispania yapinga kushiriki vikosi maalumu vya wanamaji vya Ulaya katika Muungano wa Baharini wa Marekani
Dec 28, 2023 23:00Pedro Sanchez Waziri Mkuu wa Uhispania amepinga uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuunga mkono Muungano wa Baharini wa Marekani katika Bahari Nyekundu. Sanchyez amesisitiza kuwa: 'Tunapinga kutumiwa vikosi vya baharini vya Ulaya dhidi ya maharamia kwa jina la oparesheni ya "Atalanta" kwa ajili ya kulinda meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu mkabala wa mashambulizi ya Yemen.'
-
Maelfu ya Wafaransa wanaendelea kumiminika Israel kushiriki vita vya Gaza kwa maslahi ya Wazayuni
Dec 28, 2023 22:57Maelfu ya Wafaransa wanaendelea kusafiri kuelekea Israel kwa ajili ya kushiriki katika vita vya jeshi la utawala huo haramu dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.