-
OIC: Kutotekeleza majukumu yake jamii ya kimataifa; sababu ya kuongezeka jinai za utawala wa Kizayuni
Jun 23, 2023 04:27Jumuiya ya Ushirikiano wa nchi za Kiislamu (OIC) imelaani jinai za utawala wa Kizayuni katika baadhi ya vijiji vya Palestina na kusema: Hatua ya jamii ya kimatifa ya kutotekeleza na kufungamana na majukumu yake ni sababu ya kuendelea na kuongezeka jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Ansarullah ya Yemen na Saudi Arabia zabadilishana miili wakati wa mazungumzo ya amani
Jun 23, 2023 04:11Harakati ya Ansarullah ya Yemen na Saudi Arabia zimebadilishana miili ya wapiganaji waliofariki katika mapigano ya pande mbili kama ishara ya hivi karibuni ya maendeleo katika mazungumzo yenye lengo la kumaliza uvamizi wa Saudia katika nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
-
Jeshi la Israel lawaua shahidi Wapalestina 3 kwa droni Ukingo wa Magharibi
Jun 22, 2023 03:24Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limeendeleza umwagaji damu kwa kuwaua shahidi Wapalestina watatu katika shambulizi la ndege isiyo na rubani (droni) huko kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
-
Wazayuni kadhaa waangamizwa katika shambulizi la kulipiza kisasi
Jun 21, 2023 08:38Makundi ya muqawama ya Palestina yamefanya operesheni ya ulipizaji kisasi na kuwaangamiza Wazayuni wanne na kujeruhi wengine wanne karibu na Ramallah katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
-
Kudhalilishwa jeshi la Israel huko Jenin, ukurasa mpya katika kitabu cha mapambano ya Palestina
Jun 21, 2023 08:06Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel majuzi walilazimika kutumia jeshi la anga kushambulia kwa mabomu wanaharakati wa Kipalestina katika mji wa Jenin ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
-
Al Nakhalah: Iran kamwe haiwezi kuliacha mkono taifa la Palestina mbele ya jinai za Israel
Jun 20, 2023 06:37Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amezungumzia uungaji mkono mbalimbali wa Tehran kwa muqawama wa wananchi wa Palestina na kusema kuwa, jinai zilizofanywa na wanajeshi wa Israel huko Jenin zimethibitisha kwamba medani ya mapambano za makundi yote ya muqawama ni moja.
-
Lieberman atoa wito wa kurejeshwa kwa sera ya mauaji ya kigaidi Ukanda wa Gaza
Jun 20, 2023 04:06Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amelitaka jeshi la utawala huo kutekeleza tena sera ya kuwaua kigaidi makamanda wa harakati za mapambano ya ukombozii ya Palestina katika Ukanda wa Gaza na kutekeleza operesheni kubwa za kijeshi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Wazayuni: Mapigano yalikuwa makali Jenin, tumehisi kama tunakabiliana na Hizbullah ya Lebanon
Jun 19, 2023 23:46Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimelazimika kukiri kwamba mapambano yaliyotokea jana Jumatatu kwenye mji wa Jenin huko Palestina yalikuwa tata na ya kipekee kutoka kwa wanamapambano wa Palestina.
-
Qatar na Imarati zarejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia, mabalozi wa pande mbili waanza kazi
Jun 19, 2023 23:44Qatar na Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) zimetangaza kurejesha kikamilifu uhusiano wao wa kidiplomasia na tayari mabalozi wa pande hizo mbili wameanza kazi.
-
Kuzidi kutengwa Israel sambamba na kuundwa mhimili wa Tehran-Riyadh
Jun 19, 2023 23:44Faisal bin Farhan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa saudi Arabia alisema hivi karibuni katika mazungumzo yake na Rais Rais Ibrahim Rais wa Iran kwamba: Baadhi ya nchi duniani hazitaki kuona eneo letu linapata amani na maendeleo.