-
Safari ya ujumbe wa Saudia Sana'a; dalili ya kuwepo nia ya dhati ya kuhitimisha vita vya Yemen
Apr 10, 2023 04:47Siku ya Jumamosi tarehe 8 Aprili, ujumbe wa Saudi Arabia uliwasili Sana'a mji mkuu wa Yemen, ambako ulikutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen.
-
Chanzo cha usalama Iraq kimeonya: Daesh wanarejeshwa al Anbar chini ya usimamizi wa Marekani
Apr 10, 2023 04:22Chanzo cha ngazi za juu cha usalama katika mkoa wa al Anbar nchini Iraq kimetangaza kwamba maafisa wa serikali ya nchi hiyo wanapaswa kuwa na wasiwasi wa kujirudia hali ya mwaka 2014 magharibi mwa mkoa huo na kurudi kwa wapiganaji wa kundi la Daesh (ISIS).
-
Ujumbe wa Oman wawasili Sana'a kufanikisha mapatano mapya ya kusitisha vita
Apr 09, 2023 04:52Ujumbe wa Oman umewasili Sana'a mji mkuu wa Yemen katika jitihada za kufanikisha mapatano mapya ya usitishaji vita kati ya harakati ya Ansarullah na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia. Muungano huo umekuwa ukiendesha vita huko Yemen tangu mwaka 2015.
-
OIC yatoa taarifa tena kuhusu yanayojiri Baitul Muqaddas na Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa
Apr 08, 2023 22:47Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kwa mara nyingine tena imelaani sera na hatua zote zinazochukuliwa na utawala vamizi na wa Kizayuni wa Israel kwa lengo la kufuta utambulisho wa mji mtukufu wa Baitul Muqaddas na kusisitiza kuwa, Msikiti wa Al-Aqsa ni mahala pa ibada kwa Waislamu peke yao na hatua za Wazayuni maghasibu zitavuruga amani na usalama wa eneo.
-
Qari wa Iran aibuka mshindi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Saudi Arabia
Apr 08, 2023 08:16Qari Yunes Shahmoradi kutoka Iran ameibuka mshindi katika toleo la pili la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.
-
Ansarullah yaitaka UAE kuondoa wanajeshi wake Yemen baada ya uamuzi wa Saudi wa kusitisha vita
Apr 08, 2023 07:30Mwanachama wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unapaswa kuondoa wanajeshi wake kutoka Yemen baada ya Saudi Arabia kulifahamisha Baraza la Uongozi Yemen kuhusu uamuzi wa kuhitimisha vita vya miaka minane vilivyosababisha uharibifu mkubwa nchini humo.
-
Sisitizo la Iran kuhusu ulazima wa kuwepo umoja wa Umma wa Kiislamu ili kukabiliana na jinai za Israel
Apr 08, 2023 06:39Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutaja kuunga mkono haki za watu wa Palestina na kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni kanuni isiyobadilika katika muundo wa Umma wa Kiislamu.
-
Sayyid Nasrullah atoa mwito wa kuweko mahudhurio makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds
Apr 08, 2023 04:29Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameto mwito kwa wapenda haki kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
-
Qatar: Israel inabeba dhima ya kuenea vitendo vya utumiaji mabavu katika msikiti wa al-Aqswa
Apr 08, 2023 04:28Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unabeba dhima ya kuenea vitendo vya utumiaji mabavu katika msikiti wa al-Aqswa kutokana na hatua za kichochezi za utawala huo vamizi
-
Mkuu wa CIA: Marekani imesikitishwa na kuboreka uhusiano wa Saudia na Iran, Syria
Apr 07, 2023 03:56Mkurugenzi wa Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani, CIA, William Burns ameripotiwa kusikitishwa na hatua ya Saudi Arabia kufikia mapatano ya kurejesha uhusiano na Iran na Syria huku weledi wa mambi wakiashiria kupungua kwa ushawishi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi.