-
Viongozi wa dunia walaani uvamizi wa Israel kwenye Msikiti wa al-Aqsa
Apr 07, 2023 03:54Viongozi wa dunia wameendelea kullaani vikali hujuma ya wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina katika Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) Mashariki unoalokaliwa kwa mabavu na utawala huo, wakionya kwamba hatua hiyo inaweza kuzidisha hali ya wasiwasi na taharuki.
-
Askofu: Shambulio dhidi ya Waislamu katika al-Aqsa ni sawa na kuwashambulia Wakristo
Apr 07, 2023 03:35Askofu Mkuu wa Palestina wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki huko al-Quds (Jerusalem) amelaani uchokozi usiokoma unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya waumini katika Msikiti wa al-Aqsa, huku akionyesha mshikamano wake na Waislamu wanaopambana na utawala huo ghasibu.
-
Israel yashambulia Gaza, Lebanon baada ya ulipizaji kisasi cha hujuma dhidi ya al-Aqsa
Apr 06, 2023 23:34Jeshi la utawala katili wa Israel lilishambulia maeneo ya Lebanon na Palestina katika Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa, kufuatia kuvurumishwa makombora ya kulipiza kisasi kutoka Gaza na Kusini mwa Lebanon kutokana na mashambulizi ya kinyama ya utawala huo dhidi ya waumini wa Kipalestina ndani ya Msikiti wa al-Aqsa katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds (Jerusalem).
-
Rais wa Iran atoa wito wa mkutano wa dharura wa OIC baada ya Israel kuvamia Msikiti wa al-Aqsa
Apr 06, 2023 23:11Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi ametoa wito wa kufanyika mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ili kujadili hali ilivyo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, baada ya askari wa utawala haramu wa Israel kuvamia Msikiti wa al-Aqsa na kuwalenga waumini wa Kipalestina kwa guruneti.
-
Mufti wa Oman asisitiza udharura wa kuungwa mkono Wapalestina ili kuzuia hujuma za Wazayuni
Apr 06, 2023 22:51Mufti wa Oman ametoa amepinga vikali hujuma zinazoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na ametaoa wito wa kuungwa mkono Palestina.
-
Kuongezwa kiwango cha uhusiano wa Tunisia na Syria; kutoka uwakilishi hadi balozi kamili
Apr 06, 2023 22:50Syria imepongeza uamuzi wa Rais Kais Saied wa Tunisia wa kuongeza kiwango cha uhusiano na ushirikiano wa kidiplomasia katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Damascus Syria.
-
Nchi za Kiarabu zaitisha kikao cha dharura kulaani uvamizi wa Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa
Apr 06, 2023 04:59Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelaani vikali hujuma ya hivi karibuni zaidi ya utawala haramu Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa katika Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Jumuiya hiyo pia limelaani hujuma ya kikatili ya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa katika msikiti huo kwa ajili ya ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Palestina: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa wakati na eneo
Apr 06, 2023 03:55Mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa sura ya muda maalumu wa utumiaji na sehemu maalumu ya kutumia jambo ambalo wavamizi na walowezi wa Kizayuni wanapigania kulilazimisha liwe.
-
Wairaqi zaidi ya milioni moja wametoweka na hawajulikani waliko
Apr 05, 2023 07:55Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kuwa, zaidi ya watu milioni moja wametoweka nchini Iraq na hawajulikani waliko; katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita, ikiwa ni pamoja na enzi za udikteta wa Saddam Hussein, za uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani, na za kuibuka kwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).
-
Kwa nini Israel inaogopa kuboreshwa uhusiano kati ya Iran, Syria na nchi za Kiarabu?
Apr 05, 2023 06:41Kuboreka uhusiano kati ya Syria na nchi za Kiarabu katika siku za hivi karibuni, hasa na Saudi Arabia, ambako kumefungua mlango wa kushiriki Rais wa Syria, Bashar Assad, katika mkutano ujao wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) huko Riyadh, kumeitia kiwewe na wasiwasi wa utawala ghasibu wa Israel.