Asia Magharibi
  • Hamas: Israel lazima igharamie ujenzi mpya wa Gaza

    Hamas: Israel lazima igharamie ujenzi mpya wa Gaza

    Oct 21, 2025 08:01

    Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, Mousa Abu Marzouk ametoa wito kwa Israel kufadhili kikamilifu ukarabati na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza, akitaja uharibifu mkubwa na haki za Wapalestina zaidi ya milioni mbili ambao wamepoteza makazi yao, makazi na riziki.

  • Hizbullah: Trump anajiona mtu wa amani ilhali ni gaidi namba moja duniani

    Hizbullah: Trump anajiona mtu wa amani ilhali ni gaidi namba moja duniani

    Oct 21, 2025 03:32

    Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Siasa la Hizbullah amesisitiza kuwa, Rais wa Marekani anajiona ni “mtu wa amani” duniani ilhali kiuhalisia yeye ni “mchekeshaji, muigizaji, mdanganyifu na mzandiki, na ndiye gaidi namba moja duniani” aliyemuua shahidi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah (Radhi za Allah ziwe juu yake), kwa mabomu ya Marekani.

  • Amir wa Qatar: Vita vya Israel dhidi ya Ghaza si kingine chochote ila ni mauaji ya kimbari

    Amir wa Qatar: Vita vya Israel dhidi ya Ghaza si kingine chochote ila ni mauaji ya kimbari

    Oct 21, 2025 03:30

    Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amesema, vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza si kitu kingine ila ni mauaji ya kimbari sambamba na kuulaani utawala huo ghasibu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.

  • Netanyahu ajigamba kuwa siku ya Jumapili Israel iliidondoshea Ghaza tani 153 za mabomu

    Netanyahu ajigamba kuwa siku ya Jumapili Israel iliidondoshea Ghaza tani 153 za mabomu

    Oct 21, 2025 03:30

    Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amejigamba kuwa jeshi lake lilishambulia Ukanda wa Ghaza siku ya Jumapili kwa tani 153 za mabomu, ambayo ni sawa na kukiri kwamba utawala huo ghasibu umekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano uliyofikia na harakati ya Hamas kupitia mpango uliopendekezwa na Rais wa Marekani.

  • HAMAS yaimarisha nguvu na udhibiti wake Ghaza

    HAMAS yaimarisha nguvu na udhibiti wake Ghaza

    Oct 20, 2025 23:52

    Vyombo vya usalama vya Israel vimetangaza kuwa Hamas imekuwa ikiimarisha udhibiti wake katika Ukanda wa Ghaza tangu dakika za mwanzo za kusitishwa mapigano na inaendelea kurejesha utulivu na usalama katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo, licha ya uharibifu na jinai kubwa za miaka miwili zilizofanywa na utawala wa Kizayuni kwenye eneo hilo.

  • Mufti wa Oman aunga mkono utayarifu wa Wayemen kukabiliana na Israel

    Mufti wa Oman aunga mkono utayarifu wa Wayemen kukabiliana na Israel

    Oct 20, 2025 23:30

    Mufti wa Oman ametangaza himaya na uungaji mkono wake kikamilifu utayarifu wa Wayemen kukabiliana na utawala haramu wa Israel.

  • Kushner: Hamas 'inatekeleza kwa nia njema' makubaliano ya usitishaji vita Ghaza

    Kushner: Hamas 'inatekeleza kwa nia njema' makubaliano ya usitishaji vita Ghaza

    Oct 20, 2025 07:15

    Mkwe wa Rais Donald Trump wa Marekani, Jared Kushner, ambaye ni mmoja wa wapatanishi wake wakuu katika mpango wa kusitisha mapigano Ghaza, amesema harakati ya Palestina ya Hamas imekuwa "ikitekeleza kwa nia njema" makubaliano hayo, akiashiria taarifa zilizopokelewa kutoka kwa wapatanishi wa kikanda waliohusika katika mazungumzo ya usitishaji huo wa vita.

  • Mwakilishi wa US adai vita vya Israel dhidi ya Lebanon haviepukiki ikiwa Hizbullah haitapokonywa silaha

    Mwakilishi wa US adai vita vya Israel dhidi ya Lebanon haviepukiki ikiwa Hizbullah haitapokonywa silaha

    Oct 20, 2025 06:10

    Tom Barrack, balozi wa Marekani nchini Uturuki na mjumbe maalumu wa masuala ya Syria, ametoa onyo la kutisha kwa Lebanon akiitaka ama iipokonye silaha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchi hiyo Hizbulla au ikabiliwe na mashambulizi mengine ya Israel na migogoro ya kiuchumi na kisiasa.

  • Idara ya Vyombo vya Habari vya Serikali Gaza yasajili ukiukaji 80 wa Israel tangu kusitishwa mapigano

    Idara ya Vyombo vya Habari vya Serikali Gaza yasajili ukiukaji 80 wa Israel tangu kusitishwa mapigano

    Oct 20, 2025 03:08

    Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali katika Ukanda wa Gaza imesema ukiukaji wa Israeli wa mapatano ya kusitisha vita unaakisi hamu ya utawaka huo vamizi ya kuzidisha machafuko na mtazamo wake wa kichokozi dhidi ya watu wa ukanda huo.