-
Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman
Nov 07, 2022 05:40Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na watoto wadogo.
-
Utawala wa Saudia wapanga kuwaua vijana 8 kutokana na tuhuma za ugaidi za uwongo
Nov 06, 2022 23:14Wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kwamba Ufalme wa Saudi Arabia unapanga kuwanyonga vijana wanane kutoka eneo la Qatif lenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia katika Mkoa wa Mashariki, huku ufalme huo wa kikoo unaoongozwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman ukishadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wanaotetea haki za kisiasa na kidini.
-
Jordan yaonya kuhusu hatua za Israel za kuzusha mizozo Palestina
Nov 06, 2022 23:14Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jordan ameonya kuhusiana na hatua za utawala haramu za Israel za kuzusha mivutano na mifarakano dhidi ya Wapalestina.
-
Safari ya Papa na mchezo mpya wa Al Khalifa; Uvumilivu kwa wasio Waislamu na ukatili dhidi ya Waislamu wa Bahrain
Nov 06, 2022 22:45Safari ya Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis, nchini Bahrain kwa ajili eti ya kushiriki katika mkutano wa "Amani na Kuishi Pamoja" imefanyika katika hali ambayo hakushuhudiwi amani wala kuishi pamoja kwa usalama nchini Bahrain.
-
HAMAS: Msikiti wa Aqsa uko chini ya dhulma kubwa ya Wazayuni
Nov 05, 2022 22:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa (ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu) ni miongoni mwa nembo kuu ya Uislamu na kwamba mji mtakatifu wa Quds uliko Msikiti huo mtakatifu, daima umekuwa ukilengwa na maadui Wazayuni.
-
Imran Khan: Waziri Mkuu wa Pakistan amehusika na njama ya kutaka kuniua
Nov 05, 2022 07:48Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan amemtuhumu mfuatizi wake kuwa amehusika katika njama ya kutaka kumuua.
-
Vyombo vya habari vya Israel: Miaka 25 ijayo, utawala wa Kizayuni utakuwa umeshatoweka
Nov 05, 2022 07:31Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa Israel yanaonyesha kuwa theluthi moja ya walowezi wa Kizayuni hawataki kuajiriwa jeshini na wanaamini kuwa nchi iitwayo Israel haitakuwepo tena baada ya miaka 25.
-
Wapinzani Bahrain wasema Utawala wa Al Khalifah unatumia ziara ya Papa kuficha jinai
Nov 05, 2022 04:35Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya Al-Wefaq ambayo ni kundi kuu la upinzani nchini Bahrain inasema utawala wa ukoo wa Aal Khalifah unatumia vibaya ziara ya Papa Francis nchini humo ili kuficha jinai zake na ukiukaji wa haki za binadamu.
-
Chuo Kikuu cha al-Azhar chatoa mwito wa kuweko mazungumzo ya Maulamaa wa Kishia na Kisuni
Nov 04, 2022 23:29Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimetoa mwito wa kufanyika mazungumzo baina ya Maulamaa wa Kishia na Kisuni kwa ajili ya kukabiliana na fitina na mapigano ya kikaumu.
-
Ushindi wa mafashisti katika uchaguzi wa Israel unasadifiana na maadhimisho ya miaka 100 ya Azimio la Balfour
Nov 04, 2022 23:10Uchaguzi wa hivi majuzi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel, ambao ulifanyika tarehe 1 Novemba 2022, una sifa zinazoutofautisha na chaguzi zilizopita.