-
Ndege ya kwanza ya moja kwa moja kutoka Saudia kutua Israel
Oct 25, 2021 07:47Kwa mara ya kwanza, ndege ya moja kwa moja kutoka Saudi Arabia inatazamiwa kutua usiku huu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Umoja wa Mataifa: Mamilioni ya wananchi wa Afghanistan wana hali mbaya ya kukosa chakula
Oct 25, 2021 07:22Mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yametangaza kuwa, zaidi ya nusu ya wananchi wa Afghanistan wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula.
-
Yemen yakosoa nafasi hasi ya Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa nchi hiyo
Oct 25, 2021 04:24Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amemtumia ujumbe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kukosoa msimamo wa umoja huo mkabala na mgogoro wa nchi hiyo.
-
Hivi ndivyo majeshi ya Yemen yalivyoendesha operesheni ya ukombozi wa kilomia 3200
Oct 24, 2021 23:04Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ametoa ufafanuzi kuhusu operesheni ya "Machipuo ya Ushindi" katika mikoa ya Shabwa na Ma'rib iliyofanikisha kukombolewa kilomita 3200 za ardhi ya Yemen.
-
Sisitizo la Pakistan la kutokuweko makubaliano baina yake na Marekani ya operesheni za kijeshi nchini Afghanistan
Oct 24, 2021 23:01Serikali ya Pakistan imekanusha ripoti za vyombo vya habari zinazoeleza kufikiwa makubaliano kati yake na Marekani kwa ajili ya kufanya operesheni za kijeshi na kijasusi nchini Afghanistan.
-
Hizbullah: Tutawaadhibu waliohusika na ghasia za umwagaji damu Beirut
Oct 24, 2021 11:44Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amemkosoa vikali Jaji Tarek Bitar anayeongoza uchunguzi wa mlipuko uliotokea mwaka jana katika Bandari ya Beirut na kusisitiza kuwa, hakimu huyo anapaswa kutimuliwa kwa kuwa anaingiza siasa kwenye kadhia hiyo.
-
HAMAS yaitaka tena Saudi Arabia iwaachilie huru mahabusu wa Kipalestina
Oct 24, 2021 01:05Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) kwa mara nyingine tena imeutaka utawala wa Saudi Arabia uwaachilie huru mahabusu wote Wapalestina inaowashikilia na kufunga mafaili yao.
-
Haniya: Hatutaghafilika na jukumu tulilonalo la kuwakomboa mateka wa Palestina
Oct 23, 2021 04:42Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMS amesisitiza kuwa harakati hiyo haitaghafilika na jukumu ililonalo kuhusiana na mateka Wapalestina.
-
Baraza la tume ya uchaguzi Iraq lapinga kura kuhesabiwa tena kwa mkono
Oct 23, 2021 04:19Baraza la tume ya uchaguzi ya Iraq limekataa kura za uchaguzi katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo zihesabiwe tena kwa mkono licha ya kuthibitisha kuwa kuna makosa na kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi huo.
-
Nasrullah: Imam Khomeini ameyageuza Maulidi ya Mtume (SAW) kuwa nukta ya umoja baina ya Waislamu
Oct 22, 2021 22:55Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuhusu mchango usio na kifani wa Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA) wa kuleta umoja kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni.