-
Uturuki: Tuna haki kama zilivyo Russia na Marekani ya kuwepo kijeshi nchini Syria
Oct 02, 2021 08:52Msemaji wa rais wa Uturuki amedai kuwa, nchi hiyo, kama zilivyo Russia na Marekani, ina haki ya kuwepo kijeshi katika ardhi ya Syria.
-
Miaka 21 baada ya Oktoba Mosi 2000; ibra na mazingatio ya Intifadha ya al-Aqswa kwa Wapalestina
Oct 02, 2021 08:22Wananchi wa Palestina wamefanya maandamano kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 21 ya Intifadha ya Quds ambapo wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa nara za kulaani siasa na jinai za utawala vamizi wa Quds.
-
OIC yalaani uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa
Oct 02, 2021 04:43Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani uvamizi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa.
-
Maelfu ya Wapalestina wasali Sala ya Ijumaa Quds licha hatua kali za Israel za kuwazuia
Oct 01, 2021 23:05Wapalestina wapatao 50,000 jana walisali Sala ya Ijumaa katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa licha ya hatua kali za jeshi la utawala haramu wa Israel la kuwazuia waumini kuingia katika kibla hicho cha kwanza chah Waislamu.
-
Shirika la ujasusi la Kizayuni lafungua ofisi yake ya uwakilishi Abu Dhabi, UAE
Oct 01, 2021 09:59Duru za habari zimeripoti kuwa, shirika moja la kizayuni linalotengeneza vifaa vya intaneti vya ujasusi limefungua ofisi yake mjini Abu Dhabi, katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
-
Wabahrain waandamana kupinga waziri wa utawala wa Kizayuni kukanyaga ardhi ya nchi yao
Sep 30, 2021 22:57Wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa katika miji kadhaa ya nchi hiyo kupinga waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kukanyaga ardhi ya nchi yao na kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Tel Aviv.
-
Muhammad Abdusalam: Anayetaka suluhu akomeshe vita na kuondoka katika ardhi ya Yemen
Sep 30, 2021 22:56Msemaji na mkuu wa ujumbe wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo amesema, yeyote anayetaka suluhu inampasa azikubali hatua za kuifikia suluhu, ikiwemo kukomesha uchokozi wa kijeshi, kuondoa mzingiro na kuvihamisha vikosi vyake vya kijeshi katika ardhi ya Yemen.
-
Kukiri Israel udhaifu wa "Ngao ya Chuma" na kutoweza kwake kujilinda na makombora ya Wapalestina
Sep 30, 2021 09:12Kamanda wa ulinzi wa anga wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba, mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya makombora uliopachikwa jina la "Ngao ya Chuma" hauwezi kudhamini usalama wa utawala huo mbele ya vipigo vya makombora kutoka kwa wanamuqawama wa Palestina.
-
Balozi wa Palestina UN: Israel inapanua kwa siri mpango wake wa silaha za nyuklia
Sep 30, 2021 00:13Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukipanua kwa siri mpango wake wa silaha za nyuklia na unafanya njama za kukwamisha uhudi za kupatikana eneo lisilo na silaha za nyuklia Asia Magharibi.
-
Gazeti lafichua waraka wa siri wa njama ya Imarati ya kuibana na kuidhoofisha HAMAS
Sep 29, 2021 09:31Gazeti la al Akhbar linalochapishwa nchini Lebanon limefichua waraka wa siri unaohusu mpango wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wa kuanzisha muungano dhidi ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.