-
Wanawake wa Kipalestina zaidi ya elfu 15 watiwa mbaroni na Israel kuanzia mwaka 1967 hadi sasa
Nov 26, 2020 01:04Kituo kimoja cha Utafiti Maalumu wa Masuala ya Mateka wa Kipalestina kimeripoti kuwa, zaidi ya wanawake wa Kipalestina elfu 15 wametiwa mbaroni na utawala wa Kizayuni tangu mwaka 1967 hadi sasa.
-
Malengo ya habari zenye mgongano kuhusu safari ya Netanyahu Saudi Arabia
Nov 25, 2020 21:21Katika muda wa masaa 48 yaliyopita zimetangazwa habari kadhaa zenye kugongana kuhusu safari inayodaiwa kufanywa na waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu nchini Saudi Arabia na kikao cha pande tatu kilichodaiwa kufanywa baina yake na mrithi wa ufalme wa nchi hiyo Mohammad bin Salman pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo.
-
Imarati yasitisha kutoa visa kwa raia wa nchi 13 zikiwemo Kenya na Iran
Nov 25, 2020 08:48Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umesitisha kutoa visa ya kuingia nchini humo kwa raia wanaotoka katika nchi 13 ambapo akthari ya mataifa hayo ni ya Kiislamu.
-
HAMAS: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kunashajiisha kushambuliwa Waislamu
Nov 25, 2020 08:47Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa radiamali yake kwa mashambulio ya utawala haramu wa Israel kusini mwa Syria na kusema kuwa, kuanzisha baadhi ya mataifa ya Kiarabu uhusiano wa kawaida na Wazayuni ndio chimbuko la hujuma na mashambulio haya.
-
Ansarullah: Jibu lijalo la Wayemen kwa wavamizi litakuwa kali zaidi
Nov 25, 2020 04:39Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeonya kuwa jibu lijalo litakalotolewa kwa Wasaudia wavamizi litakuwa kali zaidi na pia kubwa zaidi kuliko la kiwanda cha kusafisha mafuta cha Aramco.
-
Ni kioja cha historia wamwaga damu za wasio na hatia kupendekezewa tuzo ya amani ya Nobel
Nov 25, 2020 04:34Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni unaoteketeza roho za watoto Wapalestina na Mohammad bin Zayed al Nahyan, mrithi wa ufalme wa Imarati ambaye mikono yake imetapakaa damu za maelfu ya Wayemen wamependekezwa na mshindi mmoja wa tuzo ya Nobel kutunukiwa tuzo hiyo ya amani.
-
Jordan yaitaka jamii ya kimataifa iishinikize Israel ili isitishe ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
Nov 24, 2020 23:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jordan amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuafikii ujenzi wa nyumba mpya 540 katika eneo la Quds Mashariki unalolikalia kwa mabavu na kuitaka jamii ya kimataifa iushinikize utawala huo ghasibu ili usitishe ujenzi wake wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.
-
Kuondoka askari wa Marekani nchini Iraq; msimamo wa serikali ya Baghdad na makundi ya mapambano
Nov 24, 2020 23:12Katika hali ambayo viongozi wa serikali ya Baghdad wanasema kuwa askari 500 wa Marekani wataanza kutoka katika ardhi ya Iraq miezi miwili ijayo, Sheikh Qais al-Khaz'ali, Katibu Mkuu wa Harakati ya Asaib Ahlul Haq, karibuni hivi alitetea silaha za harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu akisisitiza kuwa muhula wa usitishaji vita na Marekani umekwisha.
-
Unicef kugawa dozi bilioni 2 za chanjo ya corona kwa nchi maskini duniani
Nov 23, 2020 09:30Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangza kuwa unataraji kugawa dozi bilioni mbili za chanjo ya maradhi ya Covid-19 kwa nchi maskini duniani.
-
WHO yatahadharisha kuhusu kusambaratika mfumo wa afya Ukanda wa Ghaza
Nov 23, 2020 09:26Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ukanda wa Ghaza ametahadharisha juu ya kusambaratika mfumo wa afya katika eneo la Ghaza.