-
Jinai kwa kinga; je, utawala wa Kizayuni unakanyaga vipi sheria za vita?
Sep 18, 2025 23:03Katika taarifa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali shambulio la jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia karibu na hospitali ya Shafa, magharibi mwa Gaza na kulitaja kuwa jinai kubwa ya kivita.
-
Askari wanne wa utawala wa kizayuni waangamizwa, wanane wajeruhiwa kusini mwa Ghaza
Sep 18, 2025 07:12Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa wanajeshi wanne wa utawala wa kizayuni wa Israel wameangamizwa na wengine wanane wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu lililotegwa ardhini kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Balozi wa Marekani Israel: Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli katika eneo la Mashariki ya Kati
Sep 18, 2025 06:42Balozi wa Marekani katika utawala wa kizayuni wa Israel, Mike Huckabee amesema, 'pamoja na Washington kuwa na washirika na marafiki kadhaa katika eneo la Mashariki ya Kati, "Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli."
-
Israel yashadidisha mauaji dhidi ya wakazi wa Gaza; mashinikizo ya kimataifa yaongezeka dhidi yake
Sep 18, 2025 03:53Idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza inaendelea kuongezeka huku mashambulizi ya kijeshi na mauaji ya kimbari ya Israel yakiingia mwaka wa pili sasa, na hivyo kuzidisha ukosoaji kimataifa.
-
Wabunge wa UK: Vikosi vya kijeshi vitakavyoongozwa na UN vipelekwe Ghaza kuzuia mauaji ya kimbari
Sep 18, 2025 00:16Wabunge watano wa Uingereza wamemwandikia barua waziri wao wa mambo ya nje Yvette Cooper wakiitaka serikali ya London "ifuatilie kwa dharura uingiliaji kati wa kijeshi utakaoongozwa na Umoja wa Mataifa" ili kukomesha mauaji ya kimbari ya yanayofanywa na Israel huko Ghaza.
-
Papa asema, Wapalestina wanahamishwa 'kwa mara nyingine tena' katika ardhi yao, ataka vita vya Ghaza vikomeshwe
Sep 18, 2025 00:15Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV amesema Wapalestina wanaishi katika "mazingira yasiyokubalika" huku wakihamishwa kwa nguvu katika Mji wa Ghaza, wakati huu wa mashambulizi makubwa yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel.
-
Yemen yakosoa vikali Mkutano wa Doha kwa kushindwa kuchukua hatua kali dhidi ya Israel
Sep 17, 2025 09:20Serikali ya Yemen imekemea vikali viongozi wa Kiarabu na Kiislamu kwa kushindwa kuchukua hatua za kivitendo katika kuunga mkono Palestina na kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni, ikisisitiza kuwa utawala huo wa kibeberu huelewa tu lugha ya nguvu.
-
Jeshi la Israel lavamia kusini mwa Syria baada ya 'makubaliano ya usalama' na HTS
Sep 17, 2025 08:31Jeshi la Israel limefanya uvamizi wa ardhini katika mkoa wa Quneitra, kusini magharibi mwa Syria, licha ya mazungumzo ya moja kwa moja yanayoendelea kati ya kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) linalotawala Syria na utawala wa Israel kuhusu kile kinachodaiwa kuwa “makubaliano ya usalama.”
-
Wazayuni wakiri, mashambulizi ya makombora ya Iran yamezorotesha vibaya mno uchumi wa Israel
Sep 17, 2025 03:17Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeifichua uhakika mpya kuhusu hasara waliyopata Wazayuni katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yaliyopewa jina la "Operesheni ya Ahadi ya Tatu ya Kweli" na kusema kuwa, mashambulizi hayo yameisababishia Israel mdororo mkubwa mno wa kiuchumi.
-
Umoja wa nchi za Kiislamu, njia mwafaka ya kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 17, 2025 02:33Marais Abdel Fattah Al-Sisi wa Misri na Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamesisitiza kuwa, kuimarishwa umoja na mafungamano baina ya nchi za Kiislamu ndiyo njia mwafaka zaidi ya kukabiliana na kukariri na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.