-
Chama cha al Ghad Tunisia: Kambi ya muqawama ishirikiane vilivyo kukabiliana na Wazayuni
May 22, 2020 22:07Katibu Mkuu wa chama cha al Ghad cha Tunisia amesisitiza kuwa, ni jambo la dharura sana kuimarishwa kambi ya muqawama kadiri inavyowezekana katika kukabiliana na Wazayuni maghasibu.
-
Jihadul Islami: Iran inahimili vikwazo vya kila namna kwa ajili ya kuihami Palestina
May 22, 2020 22:06Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amegusia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaliyofanyika jana Ijumaa kote duniani na kukumbusha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejikubalisha kuhimili na kuvumilia mashinikizo na vikwazo vya kila namna vya mabeberu kwa ajili ya kuhami malengo matukufu ya Palestina.
-
Kamati za muqawama za Palestina zapongeza hotuba ya Kiongozi Muadhamu Siku ya Quds
May 22, 2020 22:05Msemaji wa Kamati za Muqawama za Palestina amesema kuwa, hotuba iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ni endelevu, ya kiwango cha juu na muhimu sana.
-
Jeshi la Lebanon: Kukombolewa kusini mwa Lebanon yalikuwa mafanikio makubwa dhidi ya Israel
May 22, 2020 08:01Kamanda Mkuu wa Jeshi la Lebanon amehutubu kwa mnasaba wa mwaka wa 20 wa kukombolewa eneo la kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu na kuongeza kwamba, lau kama si kusimama imara kwa taifa hilo, basi mafanikio hayo makubwa yasingepatikana.
-
Katibu Mkuu wa Answarulla: Siku ya Quds ni nembo ya umoja wa umma wa Kiislamu dhidi ya adui Mzayuni
May 22, 2020 06:51Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa suala la Palestina ni kadhia ya kwanza kwa ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya umoja wa umma wa Kiislamu katika kukabiliana na adui wa pamoja wa Kizayuni.
-
HAMAS: Jenerali Esmail Qaani anafuata nyayo zile zile za Qassem Soleimani katika kuitetea Palestina
May 22, 2020 06:47Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Palestina HAMAS amesisitiza kwamba msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na Palestina ungali thabiti na imara.
-
Palestina yakataa misaada ya Imarati iliyotumwa kupitia Tel Aviv
May 22, 2020 03:32Mamlaka ya Ndani ya Palestina imekataa kupokea misaaada iliyotumwa nchini humo na Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia uwanja wa ndege wa Tel Aviv.
-
Mnong'ono wa kutokomea utawala ghasibu wa Israel wasikika katika mitaa ya Tel Aviv
May 22, 2020 01:28Intifadha ya taifa la Palestina imevuka mipaka ya kijografia ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia katika hatua muhimu ambapo sasa mnong'ono wa kumalizika na kusambaratika utawala ghasibu wa Israel umeanza kusikika katika mitaa ya Tel Aviv.
-
Hotuba za viongozi wa mrengo wa Mapambano ya Kiislamu kuhusu Siku ya Kimataifa ya Quds
May 21, 2020 04:43Viongozi wa mrengo wa Mapambanoya Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi jana Jumatano na katika kukaribia maadhimisho ya mwaka wa 41 wa Siku ya Kimataifa ya Quds walitoa hotuba muhimu kuhusu siku hiyo na suala zima la Palestina.
-
Mjumbe wa UN: Israel inapaswa kuacha vitisho vya 'kupora ardhi za Wapalestina'
May 21, 2020 03:18Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Asia Magharibi ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel utupilie mbali mpango wake wa kunyakua na kuunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zingine za Palestina unazozikalia kwa mabavu.