-
Russia yatungua droni ya Ukraine iliyokusudia kushambulia kinu cha nyuklia cha Kursk
Aug 24, 2025 07:23Vikosi vya ulinzi wa anga vya Russia vimeitungua ndege isiyo na rubani ya Ukraine (Droni) iliyokuwa imekusudia kutekeleza shambulizi katika kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Kursk cha Russia (KNPP).
-
Maandamano yafanyika London kupinga mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na Israel huko Gaza
Aug 24, 2025 04:24Maandamano makubwa yamefanyika nje ya ubalozi wa utawala wa Israel mjini London, Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Hatua ya Trump dhidi ya Bolton; ulipizaji kisasi binafsi au utakaso wa kisiasa?
Aug 24, 2025 02:58Rais Donald Trump wa Marekani, daima amekuwa akimulikwa na vyombo vya habari kutokana na mtindo wake tata wa uongozi na mbinu za hujuma dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa. Mojawapo ya mifano ya wazi zaidi ya tabia hii ni hatua yake ya karibuni dhidi ya John Bolton, Mshauri wake wa zamani wa Usalama wa Taifa, ambaye amekuwa ishara ya mivutano ya ndani katika utawala wake.
-
Korea Kaskazini yaionya Korea Kusini kuhusu vitendo vya 'uchochezi'
Aug 23, 2025 23:28Korea Kaskazini imemuonya jirani yake Korea Kusini kuhusu vitendo vya 'uchochezi' na kumtaka aachane na hatua hizo kwani zitakuwa na matokeo mabaya.
-
Je, Israeli bado ni nchi ya kitaifa ya Mayahudi au ni kituo cha muda tu ambacho kinakimbiwa hata na wafuasi kindakindaki?
Aug 23, 2025 23:26Washirika wa muda mrefu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamevunja mwiko wa uungaji mkono usio na masharti kwa Tel Aviv kwa kulitambua rasmi taifa la Palestina na kulaani mienendo na sera za waziri mkuu katili wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.
-
Jenerali wa Marekani aliyesema vituo vya nyuklia vya Iran viliharibika kidogo tu atimuliwa
Aug 23, 2025 06:07Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemfukuza kazi jenerali ambaye tathmini yake ya awali ya kiintelijensia aliyotoa ilimkasirisha Rais wa nchi hiyo Donald Trump kwa kuripoti kwamba shambulio la kijeshi ililofanya Washington mwezi Juni dhidi ya vituo vya nyuklia vya lilisababisha uharibifu mdogo tu kwa vituo hivyo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi ajiuzulu, kisa mkwamo wa vikwazo dhidi ya Israel
Aug 23, 2025 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Caspar Veldkamp amejiuzulu baada ya kushindwa kupata uungwaji mkono wa baraza la mawaziri kwa vikwazo zaidi dhidi ya Israel, kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya utawala huo wa Kizayuni huko Gaza.
-
Kwa nini Rais wa Colombia ametahadharisha kuhusu njama za Marekani za kuigeuza Venezuela kuwa Syria nyingine?
Aug 23, 2025 00:28Rais wa Colombia ametahadharisha kuwa Marekani inaweza kuifanya Venezuela kuwa Syria nyingine.
-
Senegal yaitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya majaji wa ICC
Aug 23, 2025 00:23Serikali ya Senegali imeitaka Marekani iondoe vikwazo ilivyowawekea majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Rais wa Bolivia: US inatumia kisingizo cha 'vita dhidi ya mihadarati' kuidhibiti Amerika ya Latini
Aug 22, 2025 06:33Rais Luis Arce wa Bolivia amelaani hatua iliyochukuliwa hivi karibuni na Marekani ya kutuma wanajeshi wake katika Bahari ya Karibea kusini.