-
Russia yaimarisha maandalizi ya vita ya nyuklia kufuatia maagizo ya Rais Putin
Nov 09, 2025 04:07Wizara ya mambo ya nje ya Russia imeanza kuchukua hatua za kutathmini uwezo wa taifa katika nyanja za nyuklia, kufuatia maagizo ya Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov.
-
Maandamano Paris kulaani mauaji ya halaiki Sudan, UAE yashutumiwa kwa kuunga mkono RSF
Nov 09, 2025 03:56Mamia ya waandamanaji walikusanyika Jumamosi karibu na Mnara maarufu wa Eiffel mjini Paris kulaani mauaji ya halaiki yanayoendelea nchini Sudan, huku wakiishutumu serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuwafadhili na kuwapatia silaha waasi wa RSF wanaotekeleza mauaji ya raia.
-
Palestina: Hati zilizotolewa na Uturuki za kukamatwa viongozi wa Israel ni 'ushindi kwa haki'
Nov 08, 2025 23:59Palestina imesifu na kupongeza hatua ya Uturuki ya kutoa hati za kukamatwa viongozi 37 wa utawala wa kizayuni wa Israel na kuielezea kuwa ni 'ushindi kwa haki' huku ikizitolea mwito nchi zingine kufuata mfano wa Ankara.
-
Zawadi ya dola trilioni moja kwa Musk mkabala wa njaa inayowakabili Wamarekani milioni 42; Uadilifu au mkanganyiko?
Nov 08, 2025 23:20Huku mamilioni ya Wamarekani wakihangaika kumudu milo yao ya kila siku, wanahisa wa Kampuni ya Tesla wamepasisha kifurushi cha fidia ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha dola trilioni moja kwa Elon Musk. Tofauti na kukinzana huku kukubwa kati ya utajiri wa mtu mmoja na umaskini uliokithiri wa mamilioni ya watu kumefichua taswira halisi ya pengo la pato nchini Marekani.
-
Mahakama ya Uturuki yatoa waranti wa kukamatwa Netanyahu kwa kutenda jinai Gaza
Nov 08, 2025 07:04Mahakama ya Uturuki imetoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa ulinzi na maafisa wengine 35 wakuu wa Israel kwa tuhuma za "uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari."
-
Kwa nini New Delhi imekhitari sera ya kuwa karibu zaidi na Tel Aviv?
Nov 08, 2025 00:41India na utawala wa Kizayuni wa Israel zimeanzisha uhusiano mkubwa baina ya pande hizo mbili katika miaka ya hivi karibuni.
-
Utafiti: Kilimo cha mihadarati ya afyuni nchini Afghanistan kimepungua kwa 20% katika mwaka 2025
Nov 07, 2025 06:47Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Madawa ya Kulevya na Uhalifu UNODC umeonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kilimo cha mmea wa afyuni (Opium) nchini Afghanistan katika mwaka huu wa 2025, hali inayoashiria mabadiliko makubwa katika uzalishaji na biashara ya mihadarati katika ukanda huo.
-
Hasira ya Israel Kufuatia Ushindi wa Mamdani kama Meya wa New York
Nov 06, 2025 04:17Mawaziri wa utawala katili wa Israel wameonyesha ghadhabu kufuatia kuchaguliwa kwa Zohran Mamdani kuwa meya wa jiji la New York nchini Marekani, wakimshambulia kwa tuhuma mbalimbali.
-
Trump Asema Afrika Kusini Haipaswi Kuwa Katika G20, Akataa Kuhudhuria Kikao cha Johannesburg
Nov 06, 2025 04:17Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Jumatano kuwa Afrika Kusini inapaswa kuondolewa kutoka kundi la G20, na kwamba hatahudhuria mkutano ujao wa kilele nchini humo.
-
Katibu Mkuu wa UN aonya: Kikosi kitakachotumwa Ghaza lazima kiwe na "uhalali kamili wa kimataifa"
Nov 05, 2025 23:50Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa kikosi chochote cha kurejesha uthabiti na utulivu kitakachopelekwa Ukanda wa Ghaza lazima kiwe na "uhalali kamili wa kimataifa" ili kuwasaidia Wapalestina wa eneo hilo.