-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Tuzo ya Nobel imepoteza itibari kwa mpokeaji kumsifu Netanyahu
Nov 05, 2025 09:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amekosoa tuzo ya Nobel ya Amani ya mwaka 2025, na kusema tuzo hiyo imepoteza uhalali wake kutokana na kupewa kwa Maria Corina Machado, ambaye amemsifu Benjamin Netanyahu licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
-
Iran yataka UN ichukue hatua kufuatia kauli ya Trump kuhusu majaribio ya silaha za nyuklia
Nov 05, 2025 09:08Iran imetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura kufuatia kauli za “kushtua sana” zilizotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia.
-
Nigeria yapinga madai ya Trump kuhusu mauaji ya Wakristo
Nov 05, 2025 09:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mauaji ya Wakristo nchini Nigeria, akionya dhidi ya kauli zinazoweza kuchochea mgawanyiko wa kidini au kikabila nchini humo.
-
Mamdani achaguliwa Meya wa kwanza Mwislamu wa Jiji la New York katika ushindi wa kihistoria
Nov 05, 2025 03:40Zohran Mamdani mbunge Muislamu amechaguliwa kuwa Meya wa 111 wa jiji la New York, mtu wa kwanza mwenye asili ya Asia Kusini na wa kwanza aliyezaliwa barani Afrika kuongoza jiji kubwa zaidi nchini Marekani.
-
Padri Mfaransa atuhumiwa kuwadhalilisha kingono wakimbizi watoto
Nov 04, 2025 23:36Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Rabat nchini Morocco jana aliliambia shirika la habari la AFP kuwa "ameshirikiana kikamilifu" na mamlaka za Morocco na nje ya nchi baada ya kasisi wa Ufaransa kutuhumiwa kwa kuwadhalilisha kingono wakimbizi watoto huko Casablanca.
-
Trump asema siku za Rais Maduro wa Venezuela kuweko madarakani zinakaribia ukingoni
Nov 03, 2025 22:54Katika kile kinachotafsiriwa kama harakati ya kibeberu na ya kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine, Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kuwa siku za Rais Nicolas Maduro wa Venezuela kuweko madarakani zinakaribia ukingoni, huku mvutano kati ya nchi hizo mbili ukiwa unaongezeka sambamba na Washington kushamirisha kuwepo kwake kijeshi katika eneo la Carribean.
-
Marekani haina uwezo wa kukabiliana na kombora la Burevestnik la Russia
Nov 02, 2025 22:52Afisa wa zamani wa masuala ya kijasusi wa Marekani ambaye pia ni mkaguzi wa zamani wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba Marekani haina mfumo wa ulinzi wa makombora unaoweza kukabiliana na shambulio la kombora la Burevestnik la Russia.
-
Kuna taathira gani za kufukuzwa Mwanamfalme Andrew katika mfumo wa ufalme wa Uingereza?
Nov 02, 2025 08:04Mapema usiku wa Ijumaa, Kasri ya Buckingham ilitoa taarifa rasmi ikitangaza kwamba Mwanamfalme Andrew amevuliwa vyeo vyote vya kifalme, majukumu rasmi na fursa za heshima, uamuzi ambao Mfalme Charles III aliutaja kuwa "usioepukika" kwa ajili ya kuepusha taasisi ya ufalme kuzama kwenye wimbi la kutoaminika nchini Uingereza.
-
Obama: Nyakati za giza zinatawala Marekani
Nov 02, 2025 07:39Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amemkosoa vikali Donald Trump, akiutaja utawala wake kuwa ni "kielelezo cha uasi na mparaganyiko" na kuwashutumu Warepublican kwa kukaa kimya mbele ya mienendo yake ya kutowajibika.
-
Mauaji ya halaiki ya El-Fasher yachochea tena miito ya kutaka UAE isusiwe kwa kuiunga mkono RSF
Nov 02, 2025 03:19Wito wa kuususia Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na makampuni yenye mfungamano na nchi hiyo ya kifalme unazidi kuongezeka kwenye mitandao ya kijamii, ukichochewa na hasira zinazotokana na uungaji mkono wa serikali ya Abu Dhabi kwa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.