-
ISIS yasema imehusika na shambulio lililoua makumi wa Waislamu dhidi ya msikiti, Islamabad
Feb 07, 2026 05:19Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa limehusika na shambulio lililolenga msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Khadijatul Kubra mjini Islamabad huko Pakistan na kuua makumi ya watu wakati wa Swala ya Ijumaa.
-
Waziri Mkuu wa Uhispania: Lazima serikali iwalinde watoto na 'sumu' ya mitandao ya kijamii
Feb 07, 2026 02:43Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema, nguvu ya serikali ipo kuzilinda demokrasia na "mashambulizi zinayopata" na kuwalinda watoto na vijana na "ulimwengu wenye madhara makubwa, usioadhibiwa" ambavyo ndivyo imekuwa mitandao ya kijamii hivi sasa.
-
Kwa nini China inalenga kuibadilisha Dola kwa Renminbi (Yuan) katika kiwango cha kimataifa?
Feb 06, 2026 12:30Rais wa China, Xi Jinping, ametoa wito wa kuifanya Renminbi (Yuan), sarafu ya taifa hilo, kuwa sarafu ya akiba ya dunia.
-
Tabibu wa viungo: Huenda Trump akawa amebakiwa na miaka 2 hadi 4 tu ya kuishi
Feb 06, 2026 10:10Mtaalamu wa tiba ya viungo Adam James, amezungumzia baadhi ya harakati na alama za kimwili za Donald Trump na kutahadharisha kwamba, huenda rais huyo wa Marekani asiishi zaidi ya miaka miwili hadi minne tu ijayo.
-
Trump apinga wito wa Putin wa kurefusha muda wa Mkataba wa New START
Feb 06, 2026 06:22Rais wa Marekani, Donald Trump amepinga pendekezo la Rais wa Russia, Vladimir Putin la kuongezwa kwa khiari muda wa Mkataba wa New START, unaoweka mipaka ya silaha za nyuklia, ambao muda wake ulimalizika jana Alkhamisi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil: Uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa kupitia marekebisho ya Umoja wa Mataifa
Feb 06, 2026 02:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mauro Vieira, amesisitiza haja ya kuanzishwa mfumo mpya wa kimataifa unaotegemea marekebisho ya mashirika ya kimataifa yaliyopo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama la umoja huo na Shirika la Biashara Duniani.
-
UN: ISIS inasasisha mbinu zake na kuzidisha vitishio tangu katikati ya 2025
Feb 06, 2026 02:26Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu kile ulichokielezea kama ongezeko la vitishio vya kundi la Daesh (ISIS) tangu katikati ya mwaka jana, ukieleza kuwa kundi hilo limekuwa "tata zaidi".
-
Nchi wanachama Watetezi wa Mkataba wa UN zalaani hatua ya EU dhidi ya Iran
Feb 05, 2026 07:07Nchi wanachama wa Kundi la Marafiki Watetezi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa zimetoa taarifa ambayo imelaani hatua ya hivi karibuni ya Umoja wa Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jeshi Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC.
-
Russia: Mkataba wa nyuklia wa New START baina yetu na US unamalizika leo Feb. 5
Feb 05, 2026 06:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa, Mkataba wa New START, unaoweka mipaka ya silaha za nyuklia kwa madola mawili makubwa zaidi duniani yanayomiliki silaha hizo, yaani nchi hiyo na Marekani unamalizika rasmi leo tarehe 5 Februari, na kwamba hadi sasa Moscow haijapokea jibu lolote rasmi kutoka kwa Washington kuhusu kuuongezea muda mpya mkataba huo.
-
Wasomi na wanafikra duniani watangaza kumuunga mkono Ayatullah Khamenei
Feb 05, 2026 02:35Kundi la wasomi, wanafalsafa na wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali za dunia limetangaza kumuunga mkono Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, pamoja na juhudi zake za ujasiri na zenye upeo mpana katika kulinda utu wa binadamu na haki.