-
Uchunguzi wa maoni: Theluthi mbili ya Wafaransa wanaunga mkono kujiuzulu Macron
Sep 05, 2025 03:34Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa siku tatu kabla ya uwezekano wa kuanguka serikali ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, yanaonyesha kuwa karibu theluthi mbili ya Wafaransa, ambao imani yao kwa viongozi wa sasa wa kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo imepungua, wanataka Rais Emmanuel Macron ajiuzulu.
-
Ulaghai wa watawala wa Magharibi; Gaddafi alivyodanganywa na Sarkozy
Sep 04, 2025 22:48Moja ya kesi mashuhuri za ulaghai wa watawala wa nchi za Magharibi ni udanganyifu uliofanywa na Nicolas Sarkozy, rais wa zamani wa Ufaransa dhidi ya Muammar Gaddafi, dikteta wa zamani wa Libya.
-
Filamu 'Sauti ya Hind Rajab' yapokewa kwa machozi na nara za Free Palestine huko Venice
Sep 04, 2025 08:52Filamu ya drama ya matuukio ya kweli, Sauti ya Hind Rajab, inayosimulia ombi la mwisho la msichana wa miaka mitano wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza ambaye aliuawa kikatili na jeshi la Israel mwaka jana kwa kupigwa mamia ya risasi, imepokewa kwa machozi na nara za Free Palestina kwa zaidi ya dakika 23 kwenye tamasha la filamu maarufu la Venice.
-
Mwanasiasa Ufaransa atoa wito wa kufukuzwa balozi wa Israel kwa kutoa vitisho dhidi ya meli zinazoelekea Gaza
Sep 04, 2025 07:50Mwanasiasa wa Ufaransa ametoa wito wa kufukuzwa balozi wa Israel nchini humo, Joshua Zarka, baada ya kutoa tishio dhidi ya kundi la msafara wa meli zinazoelekea Gaza zikibeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kuvunja mzingiro wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo.
-
"Vikwazo vya Marekani, Ulaya vimeua watu milioni 38 tangu 1970"
Sep 04, 2025 04:12Tahariri iliyoandikwa na tovuti ya habari ya kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imekosoa muenendo wa nchi za Magharibi kutumia vikwazo kuziadhabu nchi zinazozitazama kama maadui; ikieleza kuwa, vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya vimeua watu zaidi ya milioni 38 kote duniani tangu 1970.
-
Mwandishi wa Haaretz: Donald Trump anastahili Tuzo ya Mauaji ya Kimbari, sio Tuzo ya Amani ya Nobel
Sep 04, 2025 02:21Kufuatia uvumi kuhusu uwezekano wa kutunukiwa nishani ya Amani ya Nobel kwa Rais Donald Trump wa Marekani, mwandishi mmoja Mzayuni amekosoa jinai zinazoendelea kufanyika katika Ukanda wa Gaza kwa uungaji mkono wa serikali ya Washington na kutaka rais huyo wa Marekani afunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC.
-
Sanchez: Majibu ya Ulaya kwa vita vya Gaza ni kushindwa vibaya kwa Magharibi
Sep 03, 2025 23:04Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, amekosoa vikali msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu vita vya maangamizi vya Israel huko Gaza, na kutaja majibu ya Ulaya kwa vita hivyo kuwa ni kufeli. Amesema kwamba msimamo huo wa Ulaya unadhoofisha uaminifu wa Magharibi na kushusha chini hadhi yake kimataifa kutokana na misimamo yake ya kindumakuwili kuhusiana na Gaza na Ukraine.
-
Kwa nini mgawanyiko kati ya bunge la Uingereza na serikali kuhusu mgogoro wa Gaza unaendelea?
Sep 03, 2025 23:03Wabunge wa Uingereza sanjari na kukosoa sera za serikali ya Waziri Mkuu Keir Starmer katika vita vya Gaza wameishutumu serikali ya London kwa kuilegezea Israel.
-
Chuo Kikuu cha Utrecht ni cha kwanza Magharibi kususia Israel kwa sababu ya mauaji ya kimbari Gaza
Sep 03, 2025 09:32Chuo Kikuu cha Utrecht cha Uholanzi kimekuwa taasisi ya kwanza ya kielimu katika nchi za Magharibi kuususia kikamilifu utawala dhalimu wa Israel kufuatia mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala huo huko Gaza.
-
Russia: Udikteta wa kiliberali wa Magharibi unaeneza chuki duniani
Sep 03, 2025 02:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia amesema kuwa, ‘udikteta huria wa Magharibi’ unaeneza chuki ulimwenguni kote kwa kasi ya kutisha.