-
WHO: Kujiua husababisha kifo kimoja kati ya 100 duniani
Sep 02, 2025 23:03Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, zaidi ya kifo kimoja kati ya kila vifo 100 duniani husababishwa na kujitoa uhai. Shgirika hilo limetoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kukabiliana na dharura ya afya ya akili, hasa miongoni mwa vijana.
-
Barua ya pamoja ya Iran, Russia na China yalitaka Baraza la Usalama lipinge kutekelezwa utaratibu wa Snapback
Sep 02, 2025 07:54Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, China na Russia wameandika barua ya pamoja wakipinga hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuanzisha "utaratibu wa papo kwa hapo au Snapaback " kwa ajili ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran.
-
Afghanistan yaendelea kuwasaka manusura huku walioaga dunia kufuatia zilzala nchini humo wakifika 1,100
Sep 02, 2025 07:51Idadi ya waliofariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Afghanistan imefikia 1,124. Taasisi ya Hilali Nyekundu la Afghanistan imeripoti kuwa timu za uokoaji zinaendelea kuzunguka eneo la milimani la nchi hiyo kutafuta manusura.
-
Maduro: Tutaitangaza Venezuela 'jamhuri yenye silaha' ikiwa US itatushambulia
Sep 02, 2025 03:33Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro amesema kuongezeka uwepo wa majeshi ya Marekani katika eneo la Caribbean kunalenga kuipindua serikali yake, na kusisitiza kuwa yuko tayari "kutangaza jamhuri yenye silaha" ikiwa nchi hiyo itashambuliwa na wanajeshi hao wavamizi.
-
Matokeo ya hatua ya Marekani ya kuzuia ujumbe wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa
Sep 02, 2025 00:58Katika hali ambayo haijawahi kushuhudiwa, serikali ya Marekani imebatilisha au kuwanyima viza maafisa wapatao 80 wa Palestina akiwemo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas.
-
Ubelgiji nayo kuitambua rasmi Palestina, yaamua kuiwekea Israel vikwazo
Sep 01, 2025 23:29Ubelgiji imetangaza kuwa itatambua rasmi taifa la Palestina kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baadaye mwezi huu. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Maxime Prevot.
-
Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai yalaani mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran
Sep 01, 2025 09:05Nchi wanachama za Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO), katika tamko la pamoja lililotolewa Jumatatu, zimelaani vikali mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Zaidi ya watu 800 wafariki dunia katika tetemeko la ardhi nchini Afghanistan
Sep 01, 2025 08:26Idadi ya watu waliofariki dunia nchini Afghanistan kufuatia tetemeko baya la ardhi imeongezeka na kufikia zaidi ya 800. Msemaji wa serikali ya wanamgambo wa Taliban amesema hayo na kubainisha kwamba, eneo lililoathirika zaidi ni mkoa wa Kunar.
-
Putin: Tumefikia 'maelewano' na Trump kumaliza vita vya Ukraine
Sep 01, 2025 08:25Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kuwa, alifikia "maelewano" na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpamgo wa kumaliza vita vya Ukraine, katika mkutano wao huko Alaska mwezi uliopita.
-
Colombia yapiga marufuku kikamilifu usafirishaji wa makaa ya mawe kwa utawala wa Kizayuni
Sep 01, 2025 07:42Serikali ya Colombia imetangaza kupiga marufuku kikamilifu mauzo ya makaa ya mawe ya nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni ikiwa ni sehemu ya "mchango" wa nchi hiyo "kwa amani ya dunia."