China: Tutachukua hatua muhimu kujibu vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i131844-china_tutachukua_hatua_muhimu_kujibu_vikwazo_vya_marekani_dhidi_ya_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesisitiza kuwa nchi yake itachukua hatua "muhimu" ili kulinda haki halali za makampuni na raia wa China katika kukabiliana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.
(last modified 2025-10-11T02:32:58+00:00 )
Oct 11, 2025 02:32 UTC
  • China: Tutachukua hatua muhimu kujibu vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesisitiza kuwa nchi yake itachukua hatua "muhimu" ili kulinda haki halali za makampuni na raia wa China katika kukabiliana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Guo Jiakun ameuambia mkutano wa waandishi wa habari jana mjini Beijing kwamba China italinda usalama wa nishati yake kufuatia kushtadi vikwazo vya Marekani vinavyolenga biashara ya mafuta ya Iran na viwanda vya bidhaa za mafuta vya China.

Ameongeza kuwa China mara kwa mara imepingavikali vikwazo vya upande mmoja visivyo na msingi wowote katika sheria za kimataifa na ambavyo havijapasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.  

"Tunaihimiza Marekani kuachana na maamuzi yake yasiyofaa ya kukimbilia uwekaji vikwazo," amesema Guo Jiakun. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China pia ameitaka Marekani iache kuendeleza vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya serikali ya Rais Donald Trump siku ya Alhamisi kuwawekea marufuku kali watu 100, vyombo vya usafiri wa majini kikiwemo kiwanda na kituo binafsi cha kusafisha mafuta cha China ambacho kilikuwa kikisaidia biashara ya mafuta na petrokemikali ya Iran. 

Kampuni kwa jina la Shandong Jincheng Petrochemical Group Company kampuni ya kusafisha mafuta yenye makao yake huko China ambayo Wizara ya Fedha ya Marekani imedai kuwa imenunua mamilioni ya mapipa ya mafuta ya Iran tangu mwaka 2023.