Mijumuiko ya Siku ya Quds yafanyika nchini Kenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i124506-mijumuiko_ya_siku_ya_quds_yafanyika_nchini_kenya
Maandamano na mijumuiko ya siku ya kimataifa ya Quds imefanyika maeneo mbali mbali nchini Kenya katika ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
(last modified 2025-03-29T09:20:31+00:00 )
Mar 29, 2025 08:03 UTC
  • Mijumuiko ya Siku ya Quds yafanyika nchini Kenya

Maandamano na mijumuiko ya siku ya kimataifa ya Quds imefanyika maeneo mbali mbali nchini Kenya katika ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi wanaharakati na watetezi wa Palestina wamejumuika katika kikao cha kila mwaka ambapo wamelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakitangaza kufungamana na Wapalestina wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari.

Akizungumza katika kikao hicho, mwanaharakati Dkt. Hassan Kinyua Omari, ametoa wito kwa mataifa ya Kiarabu kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Naye Hanifa Safia, mtetezi wa haki za binadamu amesisitiza kuhusu kuendeleza mapambano makubwa dhidi ya dhuluma.

Tukio hilo limeandaliwa na Harakati ya Kenya Palestine Solidarity Movement na Kenyans 4 Palestine. Tukio hilo  lilijumuisha nara na kauli mbiu kama za uhuru wa Palestina sambamba na kuukemea utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mabango na picha zilipamba ukumbi huo zikiwa na ujumbe wa kuunga mkono Palestina na nukuu kutoka kwa watu viongozi maarufu kama Mahatma Gandhi na Nelson Mandela.

Wakenya katika miji mingine kama vile Lamu na Mombasa pia wamejiunga na wenzao duniani katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Wakati huo huo harakati ya Kongamano la Mapinduzi (KLM) nchini Kenya imesema kwamba Siku ya Al-Quds ya mwaka huu inakuja katikati ya mzozo wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya Palestina, hasa katika Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 50,000—wengi wao wakiwa wanawake na watoto—wameuawa katika mauaji ya kimbari. 

 

Taarifa hiyo imesema: "Kongamano La Mapinduzi linatoa wito wafuasti wa dini zote za kiroho duniani -Wayahudi, Wakristo, Waislamu n.k., kuungana dhidi ya itikadi ya kikatili na ya kimbari ya Uzayuni.

Aidha taarifa hiyo imesema kama ambavyo mapinduzi makubwa ya Kiislamu nchini Iran yalivvyozindua Siku ya Al-Quds mwaka 1979, kizazi cha leo kinapaswa kuendana na nyakati na kuahidi kukomboa Palestina.