Amnesty International: Serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kabla ya uchaguzi mkuu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i132226-amnesty_international_serikali_ya_tanzania_imezidisha_ukandamizaji_kabla_ya_uchaguzi_mkuu
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limesema kuwa, serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kwa wakosoaji wake wa kisiasa, waandishi wa habari, asasi za kiraia, na watetezi wa haki za binadamu katika juhudi za kudumisha madaraka na kuzuia ushiriki wa raia.
(last modified 2025-10-21T02:58:04+00:00 )
Oct 21, 2025 02:58 UTC
  • Amnesty International: Serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kabla ya uchaguzi mkuu

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limesema kuwa, serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kwa wakosoaji wake wa kisiasa, waandishi wa habari, asasi za kiraia, na watetezi wa haki za binadamu katika juhudi za kudumisha madaraka na kuzuia ushiriki wa raia.

Ripoti ya Amnesty International imeeleza kuwa, uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025 nchini humo unatarajiwa kutawaliwa na chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wagombea wakuu wa vyama vya upinzani wakikumbwa na vikwazo vingi vya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuzuiawa kugombea.

Tigere Chagutah, Mkurugenzi wa Amnesty International Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, ameonya kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepoteza fursa ya mageuzi ya kidemokrasia.

Kulingana na ripoti ya Amnesty kuna matumizi mabaya ya mfumo wa sheria, hasa mashtaka ya kisiasa yanayotumika kama silaha dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa serikali inapaswa kuachia mashtaka ya kisiasa yanayotumika kama zana za ukandamizaji, kufanya uchunguzi wa kina wa matukio ya utekaji, mateso na mauaji, na kuwahukumu wahusika wote.

Hii ni ripoti ya pili ya Amnesty International katika kipindi cha mwezi mmoja dhidi ya serikali ya Tanzania.

Mwanazoni wa mwezi huu shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilitoa ripoti kama hiyo.

Mwanzoni mwa mwezi huu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikana madai kwamba ukandamizaji wa kisiasa umeongezeka nchini humo wakati taifa hilo linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Serikali ya Tanzania ilililaumu shirika hilo kwa kutoa taarifa za aina hiyo bila kuipatia serikali fursa ya kujibu.