Spika wa Bunge la Iran akiwa rubani katika safari yake Lebanon + VIDEO
(last modified 2024-10-13T12:48:36+00:00 )
Oct 13, 2024 12:48 UTC

Mohammad Bagher Ghalibaf Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) jana aliwasili Lebanon akiwa rubani wa ndege ya ujumbe wa Iran aliouongoza.

Katika video hii Spika wa Bunge la Iran anaonekana akiendesha ndege iliyotua BeirutLebanon ambapo alikutana na kuzungumza na viongozi wa Lebanon na kutangaza uungaji mkono wake kwa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kabla ya kuelekea Geneva jana jioni.

Akizungumzia uamuzi wa kuweka kando kwa muda cheo chake na kukumbuka taaluma yake ya rubani wa ndege, Qalibaf amesisitiza kuwa, alitaka kuwaonyesha maadui kwamba, viongozi wa Iran hawaogopi vitisho vyao.