Putin amwalika Pezeshkian katika mkutano wa BRICS
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i115350-putin_amwalika_pezeshkian_katika_mkutano_wa_brics
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow, Russia, amesema kuwa Rais Vladimir Putin wa Russia amemwalika Rais Masoud Pezeshkian kushiriki katika mkutano wa wakuu wa kundi la BRICS.
(last modified 2024-08-17T23:00:55+00:00 )
Aug 17, 2024 23:00 UTC
  • Putin amwalika Pezeshkian katika mkutano wa BRICS

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow, Russia, amesema kuwa Rais Vladimir Putin wa Russia amemwalika Rais Masoud Pezeshkian kushiriki katika mkutano wa wakuu wa kundi la BRICS.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Kazem Jalali balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow, ameeleza kuwa Rais Vladimir Putin amemwalika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS, mwaliko ambao umekubaliwa na Rais Pezeshkian. 

Kazem Jalali, Balozi wa Iran nchini Russia 

Balozi wa Iran mjini Moscow Russia amesema, kujiunga Iran katika kundi la BRICS, mnamo mwezi Januari mwaka huu, ni moja ya mafanikio ya diplomasia ya Iran. Balozi Jalali amesema: Iran imeshiriki katika matukio yote ta BRICS katika ngazi ya juu kutokana na Russia kuwa mwenyekiti wa kiduru wa kundi hilo na kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tehran na Moscow. 

Jalali ameongeza kuwa, katika mkutano ujao wa BRICS kutajadiliwa uwezekano wa kutiwa saini makubaliano ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia. 

BRICS ni kundi la nchi zinazoibukia kiuchumi lilianzishwa mwaka 2006 na Brazil, Russia, India na China. Mwaka 2010 Afrika Kusini ilijiunga na kundi hilo na baadaye jina la kundi hilo lilibadilishwa kutoka BRIC na kuwa BRICS.  

Mkutano ujao wa BRICS umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 2 hadi 24 mwezi Oktoba mwaka huu huko Kazan makao makuu ya Tatarstan nchini Russia.