Rais Pezeshkian: Kama Waislamu wangekuwa na umoja, Israel isingethubutu kufanya jinai yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i115596-rais_pezeshkian_kama_waislamu_wangekuwa_na_umoja_israel_isingethubutu_kufanya_jinai_yoyote
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Lau Waislamu wote wangekuwa na umoja na mshikamano, basi utawala unaokalia kwa mabavu wa Israel haungethubutu kufanya jinai hizi kubwa katika ardhi za Palestina.
(last modified 2024-08-24T09:37:31+00:00 )
Aug 24, 2024 09:37 UTC
  • Rais Pezeshkian: Kama Waislamu wangekuwa na umoja, Israel isingethubutu kufanya jinai yoyote

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Lau Waislamu wote wangekuwa na umoja na mshikamano, basi utawala unaokalia kwa mabavu wa Israel haungethubutu kufanya jinai hizi kubwa katika ardhi za Palestina.

Daktari Pezeshkiani amesema hayo leo katika hotuba yake baada ya hafla ya wajumbe wa serikali yake mpya ya kuhuisha ahadi na mapatano na misingi ya muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini katika haramu ya Imam Khomeini.

Rais Pezeshkian ameongeza: Tunaishi katika siku Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na kwa mtazamo huu, ni lazima tufuate sira na mwenendo Imamu huyu mtukufu, vinginevyo tutapotea na kupoteza njia ya  haki.  Aidha amesema, Imam Hussein alikuwa alianzisha harakti ya Ashura kwa ajili ya kupigani haki katika jamii na baina ya Umma wa Kiislamu.

Rais Masoud Pezeshkiana kkiwa katika haram ya Imamu Khomeini

 

Rais mpya wa Iran amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979, maadui walikuwa wakijaribu kuleta mgawanyiko na mpasuko katika jamii na kudhoofisha umoja wetu na mafungamano ya ndani na kwamba, adui bado yuko katika mchakato wa kufikia lengo hili na ndio maana kuna haja ya kushikamana ili adui asituhadae.

Akizungumzia jinai zinazofanywa na utawaloa wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, Rais Pezeshkian amesema: Lau Waislamu wangekuwa na umoja na mshikamano, Israel ingethubutu kufanya jinai zote hizi? Sio Wazayuni tu, bali Marekani, Ulaya na nguvu nyingine yoyote, zisingekuwa na ujasiri wa kufanya wanachofanya hivi sasa.