Jebeli: Ulimwengu unashuhudia kuporomoka kwa utawala bandia wa Kizayuni
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) amesema kuwa, hata wananchi wa Ulaya pia wametambua uwongo wa utawala ghasibu wa Israel na dunia nzima inashuhudia kuporomoka kwa utawala huo bandia.
Peyman Jabeli amesema hayo katika hafla ya kuwakumbuka waandishi wa habari 200 waliouawa shahidi Palestina kwa jina la mauaji ya simulizi, iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Radio na Televisheni.
Mkuu huyo wa IRIB sambamba na kutoa pongezi na kutoa mkono wa pole kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na Mohammad Afif msemaji wa Hizbullah aliyeuawa juzi Jumapili amesema: Mujahidina huko Gaza na Lebanon walikuwa na mujahidina wa vyombo vya habari kando yao; kama ilivyokuwa katika vita vyetu vya kujihami kutakatifu. Jebeli amekosoa vikali himaya na uungaji mkono wa madola ya Magharibi kwa utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, kama sio himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo mtenda jinai kusingebakia kitu kinachoitwa Israel.