Balozi wa Iran: Tehran yataka kulaaniwa mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya Syria
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir-Saeed Iravani amesisitiza kuwa, kuendelea mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria na kuikalia kwa mabavu Miinuko ya Golan ya Syria na utawala huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Syria yenye zaidi ya watu milioni 16 wenye uhitaji wa dharura, Tehran daima imekuwa ikisisitiza kwamba upunguzaji wowote wa vikwazo lazima ulete maboresho ya haraka, yanayoonekana. Tehran inahoji kuwa kuendelea kukaliwa ukaliaji mabavu wa vikosi vya kigeni kunadhoofisha mamlaka ya Syria na usalama wa kikanda.
Mzozo wa Syria umesababisha mateso ya kibinadamu ya muda mrefu na mivutano ya kijiografia, huku wahusika mbalimbali wa kimataifa wakihusishwa. Msimamo wa Iran unawiana na sera yake pana ya kikanda ya kupinga uingiliaji kati wa kigeni na uchokozi wa utawala wa Israel dhidi ya nchi za Kiislamu.
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa Amir-Saeed Iravani, anasisitiza kuwa vikwazo vya upande mmoja vinakiuka sheria za kimataifa na lazima viondolewe kikamilifu na sio kusimamishwa tu. Anasisitiza kuwa vikosi vyote vya kigeni lazima viondoke mara moja na kuonya dhidi ya athari ya kudhoofisha mambo nchini Syria ambayo chimbuko lake ni operesheni za kijeshi za Israel.