-
Uhusiano wa Zanzibar na Iran unazidi kuimarika + SAUTI
Oct 20, 2022 13:08Meya wa jiji la Zanzibar ameonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Dar es Salaam Tanzania na pande mbili zimehimiza mno kuendelezwa uhusiano wa damu na wa jadi baina yao. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar
-
Kumbukumbu za kuuawa shahidi Imam Ridha AS zafanyika nchini Mauritius
Sep 27, 2022 07:22Programu maalumu ya kukumbuka siku alipouawa shahidi Imam Ridha AS zimefanyika nchini Mauritius na kuhudhuriwa na masheikh wawili kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa uratibu wa ubalozi wa Iran nchini Madagascar na Kitengo cha Kimataifa cha Haram ya Imam Ridha AS.
-
"Magharibi inafanya njama za kufuta matukufu ya Kiislamu na kupandikiza upotofu wake"
Sep 27, 2022 07:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amendelea na harakati zake za kidiplomasia pembeni mwa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kuonana na kufanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje kuanzia wa mashariki hadi magharibi mwa Asia na kutoka Amerika ya Latini hadi Ulaya na Afrika.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aonana na mawaziri wenzake wa Uganda, Eritrea na Imarati
Sep 25, 2022 03:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alionana kwa nyakati tofauti na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Uganda, Eritrea na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa. Mazungumzo ya mawaziri hao yamefanyika mjini New York, Marekani.
-
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yasikitishwa na machafuko mapya ya Libya
Aug 28, 2022 06:12Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran ameelezea kusikitishwa sana na machafuko mapya ya nchini Libya na ametaka kukomeshwa mara moja mapigano hayo. Amesema, Tehran inazitaka pande hasimu kuzingatia maslahi ya taifa, usalama wa wananchi na kutatua mambo yao kwa njia ya mazungumzo.
-
Iran: Uhusiano wetu na Tanzania unazidi kustawi na kuimarika
Aug 27, 2022 07:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, uhusiano wa Tehran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unazidi kuwa imara.
-
Amir-Abdollahian asisitiza utekelezwaji mapatano ya Iran na Tanzania
Aug 27, 2022 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu utekelezwaji wa mapatano yaliyofikiwa katika kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Iran na Tanzanjia.
-
Rais wa Tanzania akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Aug 26, 2022 23:29Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian mjini Dodoma.
-
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akutana na Rais wa Zanzibar
Aug 26, 2022 05:23Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu7 ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar na wawili hao wamesitizia udharura wa kuimarishwa ushirikiano baina ya pande mbili.
-
Amir-Abdollahian: Afrika ni moja ya vipaumbele vikuu vya diplomasia ya kiuchumi ya Iran
Aug 25, 2022 06:54Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania amesema kuwa, bara la Afrika ni moja ya vipaumbele vikuu vya diplomasia ya kiuchumi ya Iran.