-
Mahakama ya Uholanzi yaiamuru Serikali isimamishe kuipatia Israel vifaa vya ndege za kivita
Feb 12, 2024 08:01Mahakama ya Uholanzi imeiamuru serikali kusitisha utoaji wa vifaa na vipuri vya ndege za kivita za F-35 zinazotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi yake ya kinyama unayofanya katika Ukanda wa Gaza.
-
Maandamano makubwa yafanyika Rabat kupinga uhusiano wa Morocco na Israel 'mfanya mauaji ya kimbari'
Feb 12, 2024 07:30Maelfu ya Wamorocco wamejitokeza tena kwenye barabara za mji mkuu wao Rabat kutoa wito wa kusitishwa uhusiano wa nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao wameulaani na kuutaja kuwa kuwa ni mfanya "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza.
-
Misri yatishia kusimamisha Mkataba wa Camp David endapo Israel itashambulia Rafah
Feb 12, 2024 06:49Misri imetishia kusitisha mkataba wa amani wa Camp David iliosaini na utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo wanajeshi wa utawala huo ghasibu watapelekwa katika mji wa mpakani wa Gaza uliofurika watu wa Rafah na kusema mapigano huko yanaweza kulazimisha kufungwa kwa njia kuu ya kusambazia misaada katika eneo hilo.
-
Hizbullah yaonya dhidi ya sera ya kupenda vita ya Israel
Feb 12, 2024 01:07Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mrengo wa muqawama haujatangaza vita kamili, lakini iwapo Israel itapanua vita vyake vya Gaza, wanamuqawama hawatasita kufanya mashambulizi ya kujibu chokochoko za adui huyo mpenda vita.
-
Iran yaonya kuhusu uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Israel
Feb 09, 2024 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya vikali Marekani dhidi ya kuendelea kuiunga mkono Israel na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.
-
Israel yaua watoto wa chekechea katika shambulio la anga Gaza
Feb 04, 2024 07:48Kwa akali watoto wawili wa Kipalestina wameuawa shahidi katika shambulizi la anga lililofanywa na ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya shule moja ya chekechea katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Wamarekani waandamana kupinga himaya ya Washington kwa jinai za Israel huko Gaza
Feb 03, 2024 08:33Wananchi wa Marekani wamefanya maandamano makubwa wakipinga uungaji mkono na himaya ya serikali ya Washington kwa jinai na mauaji yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa mara moja vita huko Palestina.
-
Hizbullah: Njia pekee ya kuondoa wasiwasi ni kukomeshwa mauaji ya kimbari Ghaza
Feb 02, 2024 23:38Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati hiyo imejiweka tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, njia pekee ya kuondoa wasiwasi uliopo ni Israel kukomesha mauaji ya watu wasio na hatia huko Ghaza, Palestina.
-
UN yailaani Israel kwa kuwaua na kuwanyamazisha waandishi wa habari huko Gaza
Feb 02, 2024 10:36Wataalamu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza kusitikishwa na kulaani vitendo vya waandishi wa habari kuuawa, kushambuliwa, kujeruhiwa na kuwekwa vizuizini na vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu la Ukanda wa Gaza.
-
WAFF yataka Israel ifukuzwe katika shughuli zote za kandanda duniani
Feb 02, 2024 04:20Shirikisho la Soka la Asia Magharibi (WAFF) limetoa mwito wa kusimamishwa utawala wa Israel katika mashindano na shughuli zote zinazohusiana na mpira wa miguu duniani, madhali Tel Aviv inaendeleza vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.