-
Maafisa Usalama Iraq wazima jaribio la shambulizi la kigaidi Karbala
Mar 29, 2021 08:04Maafisa usalama wa Iraq wamezima jaribio la shambulizi la kigaidi lililolenga mjumuiko mkubwa wa wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) uliokuwa njiani kutoka Najaf ukielekea katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa Imam wa Zama na mwokozi aliyeahidiwa wa Akheri Zamani, Imam Mahdi (as).
-
Mamilioni washiriki maombolezo ya Tasua kwa kuchunga protokali za afya
Aug 29, 2020 03:32Licha ya janga la corona, na huku wakichunga protokali za afya, mamilioni ya Waislamu wa Iran na maeneo mengine ya dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, majlisi na shughuli za maombolezo ya Tasua.
-
Zaidi ya wafanyaziara milioni 17 wameshiriki katika Arubaini ya Imam Hussein (as) ya mwaka huu
Oct 20, 2019 23:09Gavana wa mkoa wa Karbala nchini Iraq ametangaza kuwa, idadi ya mazuwari walioshiriki kwenye maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (as) mwaka huu imepindukia milioni 17.
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa familia za Mashahidi wa Karbala
Sep 11, 2019 03:05Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Iraq na familia za Mashahidi kufuatia tukio la kufa shahidi makumi ya watu katika mji mtakatifu wa Karbala.
-
Waislamu milioni tatu wazuru Haram ya Imam Hussein Karbala, wakumbuka mauaji yake
Sep 10, 2019 22:56Zaidi ya Waislamu milioni tatu jana tarehe 10 Muharram ambayo ni maarufu kama siku ya Ashura, walishiriki katika maombolezo ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume wetu muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq.
-
Wafanyaziara milioni 15 wamefika Karbala kushiriki kwenye Arubaini ya Imam Hussein (as)
Oct 30, 2018 03:56Baraza la Mkoa wa Karbala nchini Iraq limetangza kuwa limesajili wafanyaziara milioni 15 walioingia nchini humo kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein (as) huku idadi ya mazuwari hao ikiwa inaendelea kuongezeka.
-
Siku moja kabla ya Arubaini ya Imam Hussein (as) zaidi ya wafanyaziara milioni 10 wameshazuru Karbala
Oct 29, 2018 04:45Naibu Mkuu wa Mkoa wa Karbala nchini Iraq amesema: Hadi sasa zaidi ya wafanyaziara milioni 10 wamewasili mkoani humo kwa lengo la kushiriki Arubaini ya Imam Hussein (as).
-
Waombolezaji Iran, duniani wajitokeza kwa wingi kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein AS
Sep 20, 2018 03:05Mamilioni ya Waislamu katika nchi mbali mbali duniani wamejotokeza kwa mamilioni katika Siku ya Ashura kukumbuka siku alipouawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.
-
Leo ni siku ya Ashura ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume, Imam Husain AS
Sep 19, 2018 23:23Alkhamisi ya leo ya tarehe 20 Septemba 2018 Milaadia inasadifiana na mwezi kumi Muharram 1440 Hijria, siku ya Ashura ya kukumbuka alipouawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, mmoja wa mabwana wawili wa vijana wa peponi, Imam Husain AS.
-
Salum Bendera na ripoti ya kumbukumbu za Arubaini ya Imam Husain AS, Karbala Iraq
Nov 11, 2017 07:42Jana Ijumaa mwezi 20 Mfunguo Tano Safar sawa na tarehe 10 Novemba 2017 ilisadifiana na Arubaini ya Imam Husain AS kwa mujibu wa kalenda ya Iraq. Mamilioni ya Waislamu kutoka kona mbalimbali za dunia wameshiriki katika kumbukumbu hizo zilizofikia kileleni jana huko Karbala Iraq. Mwenzetu Salumu Bendedra aliyetumwa maalumu kuakisi tukio hilo ametutayarishia ripoti ifuatayo