-
Kiongozi Muadhamu aonana na matabaka mbalimbali ya wananchi wa mkoa wa Azerbaijan Mashariki
Feb 17, 2016 11:39Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi na kwa mwamko wananchi wa Iran katika chaguzi mbili zijazo za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na ule wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu la kumchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu kutabatilisha njama za maadui.
-
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Ugiriki
Feb 09, 2016 09:42Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezikosoa siasa za kindumakuwili za Marekani na kubainisha kwamba, ugaidi ni maradhi ya kuambukiza na hatari mno na kutanabihisha kwamba, inawezekana kuyadhibiti maradhi hayo ikiwa watu wote watachukua hatua za dhati za kukabiliana nayo.
-
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu katika mkutano na maafisa wa Jeshi la Anga
Feb 09, 2016 04:08Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, siku ya Jumatatu alikutana na makamanda na maafisa wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema, maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Februari 11 Bahman na uchaguzi ujao wa Februari 26 ni Idi mbili zenye maana kwa taifa la Iran.
-
Kiongozi Muadhamu: Baraza Kuu la Usalama wa Taifa linapaswa kutawaliwa na mantiki na fikra sahihi
Feb 03, 2016 10:42Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa anga inayotawala sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na maamuzi yake inapaswa kwenda sambamba na fikra sahihi, halisi za kimapinduzi na za kihizbullah.