-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Sahihi ya rais wa Marekani si ya kutegemewa
Nov 19, 2021 11:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, sharti la kukubaliwa Marekani kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni kuondoa Washington kwa namna athirifu, itakayoweza kuthibitika na kwa wakati mmoja vikwazo vyote ilivyoiwekea Iran na kwamba sahihi ya rais wa Marekani haiwezi kutegemewa.
-
"Vikwazo vipya dhidi ya Iran ni muendelezo wa sera zilizofeli za Trump"
Nov 19, 2021 04:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu si kitu kingine ghairi ya muendelezo wa sera zilizogonga ukuta za Donald Trump.
-
Ripoti: Mihadarati inaua watu zaidi ya laki 1 kila mwaka Marekani
Nov 19, 2021 04:17Ripoti mpya ya utafiti inaonesha kuwa, idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na matumizi ya mihadarati nchini Marekani imeongezeka na kupindukia watu laki moja kwa mwaka.
-
Russia yakosoa mwenendo wa kinafiki wa Marekani kuhusu masuala ya anga
Nov 18, 2021 23:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaja tuhuma za Marekani dhidi ya Moscow kwamba inatumia silaha dhidi ya satalaiti na kusababisha vitisho angani kuwa ni za kinafiki na zisizo na ukweli wowote. Sergey Lavrov amesema kuwa: "Tunaona kwkamba, badala ya kutoa madai yasiyo na msingi wowote, ni vyema Marekani iketi kwenye meza ya mazungumzo na ieleze mitazamo yake kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa na Russia na China kwa ajili ya kuzuia mashindano ya silaha angani
-
Kenya na Marekani zajadili namna ya kukomesha machafuko Sudan na Ethiopia
Nov 18, 2021 04:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru wa Kenyatta wa Kenya kujadili namna ya kuhitimisha machafuko katika nchi za Sudan na Ethiopia.
-
Marekani yaweka rekodi mbaya mpya; mara hii ni ya vifo vinavyotokana na madawa ya kulevya
Nov 18, 2021 04:15Kituo cha udhibiti na uzuiaji maradhi cha Marekani kimetangaza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, takwimu za vifo vinavyosababishwa na matumizi ya kupindukia ya madawa ya kulevya zimevuka kiwango cha watu laki moja kwa mwaka.
-
Mjumbe Maalumu wa Iran: Marekani inaunga mkono ISIS
Nov 15, 2021 08:21Mjumbe Maalum wa Rais wa Iran katika masuala ya Afghanistan amesema Marekani ilipata pigo na kushindwa vibaya huko Afghanistan, na sasa inajaribu kuliunga mkono kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).
-
Nigeria yashambulia asasi ya Marekani kwa kuipaka matope
Nov 15, 2021 08:18Serikali ya Nigeria imeijia juu asasi moja isiyo ya kiserikali ya Marekani iliyodai kuwa, utawala wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi unaunga mkono ugaidi.
-
Kufichuliwa jinai za kivita za jeshi la Marekani nchini Syria
Nov 14, 2021 07:42Gazeti la New York Times limetoa ripoti inayoonyesha kuwa, jeshi la Marekani limetenda uhalifu wa kivita kwa kuua makumi ya wanawake na watoto katika mashambulio ya anga liliyofanya nchini Syria kwa kisingizio cha kile kinachoitwa mapambano dhidi ya kundi la DAESH (ISIS).
-
Eritrea yalaani vikwazo 'haramu' vya Marekani dhidi yake
Nov 14, 2021 04:44Serikali ya Eritrea imekosoa vikali vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na ghasia na mapigano yanayoshuhudiwa katika nchi jirani ya Ethiopia.