-
CNN: Wamarekani elfu mbili wanakufa kila siku kwa virusi vya corona
Sep 20, 2021 03:31Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa, kwa wastani Wamarekani elfu mbili wanafariki dunia kila siku kutokana na virusi vya corona na kwamba idadi hiyo ndiyo ya juu zaidi tangu mwezi Machi mwaka huu.
-
Familia ya Waafghani waliouawa na Marekani: Kuungama hakutoshi, wahusika wachukuliwe hatua
Sep 19, 2021 12:03Familia ya raia kumi wa Afghanistan waliouawa katika shambulizi la ndege isiyo na rubani ya jeshi la Marekani mjini Kabul imekataa hatua ya serikali ya Washington ya kuungama na kuomba radhi kutokana mauajii hayo.
-
Washington: Kwa sasa Russia ni tishio kubwa zaidi kwa Marekani kuliko China
Sep 19, 2021 02:46Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani amedai kwamba kwa sasa Russia ni tishio kubwa kwa usalama wa nchi hiyo na Ulaya kuliko China.
-
Kushadidi mivutano baina ya Marekani na Ufaransa, Paris yamwita nyumbani balozi wake mjini Washington
Sep 18, 2021 21:52Ufaransa imechukua uamuzi wa kumwita nyumbani balozi wake mjini Washington sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa serikali ya Paris na Marekani. Vilevile imechukua hatua ya kumrejesha nyumbani balozi wake nchini Australia kama hatua ya kuonesha malalamiko yake.
-
New York Times: Hizbullah imeishinda na kutoa pigo kwa Marekani
Sep 17, 2021 22:37Gazeti la New York Times la Marekani limekiri kuwa harakati ya Hizzbullah ya Lebanon imeibuka na ushindi katika mpambano wake na Marekani.
-
Nusu ya wanunuzi wa silaha nchini Marekani ni wanawake
Sep 17, 2021 02:57Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa tangu mwaka 2019 hadi mwezi Aprili mwaka huu wanawake wameunda karibu ya nusu ya wamiliki wapya wa silaha nchini humo.
-
Waziri wa Lebanon: Mafuta ya Iran yamevunja vikwazo vya kidhalimu vya Marekani
Sep 16, 2021 07:47Waziri wa Kazi wa serikali mpya ya Lebanon amesema sambamba na kuingia misafara ya mafuta ya Iran katika ardhi ya nchi hiyo kwamba, shehena hizo za mafuta zimevunja mzingiro wa kihistoria na wa kidhalimu ambao Marekani ilikuwa imeiwekea Lebanon.
-
Faida kubwa ya mashirika ya kutengeneza silaha ya Marekani kutokana na tukio la Septemba 11
Sep 15, 2021 21:53Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Watson Institute for International and Public Affairs la Chuo Kikuu cha Brown nchini Marekani, nusu ya bejeti ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon baina ya miaka ya 2001 hadi 2020 ambayo inafikia dola trilioni 14 imewaendea wakandarasi na mashirika yanayotenegeneza silaha ya nchi hiyo. Kati ya fedha hizo dola trilioni 4.4 zilitengewa vituo vya kijeshi na viwanda vinavyohusika na masuala ya kijeshi.
-
Gazeti la Russia: Iran imefelisha njama za Marekani katika Bodi ya Magavana ya IAEA
Sep 15, 2021 01:54Gazeti la Kommersant la Russia limeandika kuwa, Iran imefelisha njama za Marekani na waitifaki wake wa Ulaya za kutaka kutoa azimio dhidi ya Tehran katika kikao cha Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Zakharova: Lengo la Marekani huko Ukraine ni kuishinikiza Russia
Sep 14, 2021 10:31Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa lengo la mpango wa Marekani eti wa kuimarisha demokrasia nchi ya Ukraine ni kuiweka chini ya mashinikizo Russia na kuyumbisha hali ya mambo katika eneo hilo.