-
Iran yavurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za jeshi za Marekani
Jan 08, 2020 00:18Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limevurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.
-
Muungano wa Marekani wahamisha makao yake makuu kutoka Iraq hadi Kuwait
Jan 07, 2020 23:21Muungano eti wa kupambana na kundi la Daesh unaoongozwa na Marekani umehamisha makao yake makuu kutoka Iraq na kuyapeleka Kuwait kufuatia mauaji ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi Abu Mahdi al Muhandes, na sisitizo la Iran la kulipiza kisasi mauaji hayo ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani.
-
Kupinga Russia na China taarifa ya upande mmoja ya Marekani kuhusiana na matukio ya Iraq
Jan 07, 2020 23:17Jinai za Marekani huko Iraq hususan shambulio lake la kijeshi dhidi ya ngome za Harakati ya Wananchi ya al-Hashd al-Shaabi katika mpaka wa pamoja wa Iraq na Syria, zimekabiliwa na malalamiko makubwa ya Wairaqi ambao walifanya maandamano na kukusanyika katika ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.
-
Marekani yamnyima Zarif viza ya kushiriki mkutano wa UN
Jan 07, 2020 04:40Marekani imekataa kumpa viza ya usafiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaotazamiwa kufanyika Januari 9 mjini New York.
-
Vitisho vya Trump vya kuiwekea vikwazo Iraq, kushindwa kwingine kwa Washington
Jan 07, 2020 04:14Jinai kubwa ya Marekani ya kumuua kigaidi Meja Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq ya Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq, imeibua radiamali kali ya bunge la nchi hiyo ya Kiarabu na kuipelekea kupitisha sheria ya kuvitimua vikosi vya muungano vamizi wa eti kupambana na Daesh (ISIS) unaojumuisha askari wa Marekani.
-
Vitisho vipya vya Trump kutokana na wahka wa ulipizaji kisasi wa Iran
Jan 05, 2020 23:13Hatua ya kijinai na iliyo kinyume cha sheria ya Marekani ya kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq pamoja na shakhsia wengine huko mjini Baghdad, imekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa Iran ambayo imesisitizia kulipiza kisasi kikali kwa Marekani.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran; Ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani
Jan 05, 2020 23:10Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Kamanda Qassem Soleimani; na watu wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao mbele ya jinai hiyo.
-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 12:26Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Ukosoaji wa Russia dhidi ya njama za Marekani za kubadili mlingano wa nguvu Asia Magharibi na kuongeza vitisho vya usalama kimataifa
Jan 05, 2020 09:51Hatua za Marekani katika eneo la Asia Magharibi hususan za kuzidisha uwepo wake kijeshi, mashinikizo dhidi ya Iran na hatimaye kutekeleza hatua za kigaidi hasa za kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la IRGC, Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes na shakhsia wengine walioambatana nao, zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa Russia kama mmoja wa wacheza karata muhimu katika eneo hili.
-
Wamarekani waandamana kulaani uchu wa vita wa utawala wa Trump
Jan 05, 2020 04:27Maelfu ya wanaharakati na wananchi wa Marekani wamefanya maandamano katika makumi ya miji ukiwemo mji mkuu Washington, kulaani hatua ya utawala wa Donald Trump ya kumuua shahidi kamanda wa jeshi la Iran, Luteni Jenerali Soleimani, pamoja na hatua ya Washington ya kutuma maelfu ya askari katika eneo la Asia Magharibi.