-
HAMAS: Kauli ya Marekani ni uongo mtupu, Wapalestina Ghaza wanauawa kwa silaha zake
Jul 26, 2024 09:29Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: "Madai ya Washington kwamba inatiwa wasiwasi na hali ya kibinadamu na inasikitishwa na machungu na mateso wanayopata watu wa Ghaza ni uongo wa Kimarekani".
-
Amnesty International: Marekani mshirika wa Israel katika mauaji ya kimbari Palestina
Jul 25, 2024 03:41Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International imeonya Marekani kuhusu kuupa silaha utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza na kutangaza kuwa, Washington ni mshirika wa utawala huo katika mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.
-
Duru mpya ya mazungumzo ya pamoja ya usalama kati ya Marekani na Iraq mjini Washington
Jul 24, 2024 07:44Alina Romanowski, balozi wa Marekani mjini Baghdad, alitangaza siku ya Jumatatu kuhusu kuanza mazungumzo kati ya Marekani na Iraq huko Washington mji mkuu wa Marekani ajenda kuu ikiwa ni "mustakabali wa muungano wa kimataifa."
-
Biden ajitoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais wa Marekani
Jul 22, 2024 22:53Hatimaye, Joe Biden, Rais wa Kidemokrati wa Marekani mwenye umri wa miaka 81, amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais wa nchi hiyo baada ya mijadala mingi kuhusu kugombea kwake katika uchaguzi wa Novemba 5 mwaka huu, na kumuunga mkono Kamala Harris, makamu wake kama mgombea wa kiti hicho.
-
Republican: Biden ni punguani, asiachiwe kitufe cha silaha za nyuklia
Jul 22, 2024 07:27Muda mfupi baada ya Rais Joe Biden wa Marekani kutangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kutetea kiti chake cha urais, viongozi waandamizi wa chama cha Republican wamesema mwanasiasa huyo mwenye miaka 81 hapasi kuachiwa nywila (kodi) za kitufe cha silaha za nyuklia kutokana na matatizo ya kisaikolojia yanayomsumbua.
-
Marekani na Ujerumani; Wauzaji silaha wakuu kwa utawala katili wa Israeli
Jul 21, 2024 03:55Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) imetangaza katika ripoti yake kwamba kati ya asilimia 99 ya silaha zilizoagizwa na utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza kati ya mwaka 2019 na 2023, asilimia 69 ilitoka Marekani na asilimia nyingine 30 kutoka Ujerumani.
-
Blinken: Kujiondoa JCPOA ni katika makosa makubwa ya Marekani
Jul 21, 2024 03:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekiri bayana kuwa, hatua ya nchi hiyo ya kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni moja ya makosa makubwa zaidi yaliyowahi kufanywa na Washington katika miaka ya hivi karibuni.
-
Kukosoa Russia upinzani wa Magharibi kwa muundo mpya wa ulimwengu
Jul 20, 2024 23:00Balozi wa Russia nchini Marekani, Anatoly Antonov, amesema nchi za Magharibi zinapinga juhudi za kuundwa muundo mpya wa pande kadhaa ambao utakuwa na insafu na uadilifu zaidi.
-
Marekani chimbuko kuu la matatizo Asia Magharibi
Jul 20, 2024 07:03Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekosoa vikali maamuzi na hatua za mabavu na za upande mmoja zinazochukuliwa na Marekani katika masuala mbali mbali ya Asia Magharibi na kubainisha kwamba, hatua hizo ndio chimbuko kuu la matatizo yanayolikumba eneo hili.
-
Wizara: Watoto wanabakwa katika kambi za wahajiri Marekani
Jul 20, 2024 02:40Imebainika kuwa, maelfu ya watoto wahajiri wamebakwa na kufanyiwa unyanyasaji na udhalilishaji wa kingono katika kambi na vituo vya 'kuwahifadhi' wahamiaji haramu nchini Marekani.